TFF YAFUNGUA DIRISHA LA USAJILI 2026/2027
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limefungua rasmi dirisha kubwa la usajili wa wachezaji kwa msimu wa 2026/2027, mchakato utakaoziweka klabu zote katika msisimko mkubwa wa kuwania saini za mastaa wapya.
Dirisha hilo lililoanza kutimua vumbi Julai 6, litafungwa rasmi Agosti 15, mwaka huu saa 5:59 usiku, huku TFF ikitoa onyo kwa klabu za Ligi Kuu ya Bara, Championship, First League, Ligi ya Vijana (U-20) na Ligi ya Wanawake kuhakikisha zinakamilisha taratibu zote mapema kwa sababu hakutakuwa na sekunde ya nyongeza.
Katika kuhakikisha uwazi na weledi, usajili na uhamisho wote utafanyika kidijitali kupitia mfumo wa FIFA Connect, ukihusisha wachezaji wapya, wanaoongeza mikataba, au wanaohama kwa mkopo na jumla.
Ili kukwepa dhoruba za kisheria na pingamizi, klabu zote zinatakiwa kupakia nyaraka zote muhimu kwenye mfumo huo, ikiwa ni pamoja na mikataba ya ajira, hati za kusafiria au vitambulisho vya uraia, barua za uhamisho, vyeti vya afya na ushahidi wa malipo ya ada ya usajili, hatua itakayozilazimu klabu kukimbizana na wakati ili kujenga vikosi imara vya msimu ujao.

Post a Comment