WAANDISHI WAASWA KUFANYA UCHUNGUZI WA KINA MASWALA YA MAENDELEO



WITO umetolewa kwa wanahabari Nchini kuendelea kufanya uchunguzi wa kina kuhusu masuala yanayohusu maendeleo ya bara la Afrika na kuhakikisha simulizi za Waafrika zinasimuliwa na Waafrika wenyewe.


Wito huo umetolewa Dar es Salaam na mwandishi wa habari za uchunguzi na mtayarishaji wa filamu ya maandishi (documentary), David Hundeyin. Alisema Waafrika wanapaswa kuelewa kwa undani sababu zinazochangia matukio ya kisiasa yanayotokea barani humo badala ya kuamini kuwa yanachochewa na sababu za ndani pekee.

Alisema kuwa baadhi ya vyombo vikubwa vya habari vya kimataifa vinaendeshwa kwa kuzingatia maslahi ya nchi vinakotoka na hivyo huwasilisha habari kwa mtazamo unaoendana na malengo ya kisiasa ya mataifa hayo.

“Waandishi wa habari wanapaswa kutambua kuwa kila chombo cha habari kina mtazamo fulani. Ni muhimu kwa Waafrika kujenga uwezo wa kusimulia hadithi zao wenyewe na kuchambua taarifa wanazopokea kutoka vyanzo mbalimbali,” amesema.


No comments