UVCCM YAKEMEA VITENDO VYA UCHOCHEZI YAPONGEZA MARIDHIANO
Baraza Kuu la Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) limepitisha maazimio matatu makubwa likiwemo la kumpongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa uongozi wake, kukemea vitendo vya uchochezi vinavyotishia amani ya nchi na kuwataka vijana kushiriki kikamilifu katika kulinda umoja na mshikamano wa Taifa.
Maazimio hayo yamepitishwa katika kikao cha kawaida cha Baraza Kuu kilichoongozwa na Mwenyekiti wa UVCCM, Mohammed Ali Kawaida, kilichofanyika katika Ukumbi wa NEC, Makao Makuu ya CCM mjini Dodoma.
Baraza pia limeipongeza Serikali ya Rais Samia kwa utekelezaji wa miradi ya kimkakati, kuimarisha uchumi, diplomasia ya kimataifa pamoja na kuboresha huduma za afya na kijamii.
Aidha, limempongeza Rais wa Zanzibar Dkt. Hussein Mwinyi kwa juhudi zake za kuimarisha maridhiano ya kisiasa visiwani Zanzibar.
Katika azimio la pili, Baraza Kuu la UVCCM limekemea kwa kauli moja vitendo vya uchochezi wa vurugu na uvunjifu wa amani vinavyodaiwa kufanywa na baadhi ya wanasiasa na wanaharakati, likisisitiza kuwa halitasita kusimama mstari wa mbele kupinga mtu au kikundi chochote kitakachohatarisha amani na utulivu wa Tanzania.

Post a Comment