'AMKENI MNATUMIKA'
Watanzania wametakiwa kuacha kusikiliza wanaharakati na wanasiasa wanaochochea vurugu na uvunjifu wa amani nchini, kwa kuwa watu hao hawana nia njema kwa taifa.
Rai hiyo imetolewa Dar es Salaam na mwanafalsafa wa Pan-Afrika kutoka Zimbabwe, Dk Joshua Maponga, wakati wa mkutano na waandishi wa habari.
Dk Maponga amesema baadhi ya mashirika yasiyo ya kiserikali (NGOs) hupokea fedha kutoka mataifa ya nje kwa lengo la kuhamasisha vitendo vinavyokwenda kinyume na maadili na amani ya nchi, akisisitiza kuwa Serikali inapaswa kufanya uhakiki wa mashirika hayo ili kubaini vyanzo vya fedha na matumizi yake.
Ameongeza kuwa wananchi wanapaswa kuwa makini na watu wanaoendelea kutumia mitandao ya kijamii kuhamasisha vurugu, akisisitiza kuwa vitendo hivyo vinaweza kuathiri maendeleo ya taifa na ustawi wa jamii kwa ujumla.
Kwa upande wake, Mtendaji Mkuu wa African Spear Head Media, David Hundeyin, amesema Tanzania ni nchi muhimu kiuchumi barani Afrika kutokana na nafasi yake ya kimkakati, hususan Bandari ya Dar es Salaam, hivyo wananchi wanapaswa kulinda amani na rasilimali za taifa ili kuepuka athari za kiuchumi na kijamii zinazoweza kusababishwa na vurugu.
.jpeg)
Post a Comment