BILA AMANI HAKUNA MAENDELEO
Katibu wa NEC,
Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Kenani Kihongosi,
amewataka wananchi wa Wilaya ya Karatu mkoani Arusha kuendelea kulinda amani na
utulivu uliopo ili kuhakikisha shughuli za kiuchumi na maendeleo zinaendelea
kustawi katika eneo hilo.
Akizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika Karatu, Kihongosi amesema
amani ndiyo nguzo kuu inayowezesha wananchi kufanya biashara, kulima, kuendesha
shughuli za utalii pamoja na kazi za usafirishaji ikiwemo bodaboda na bajaji.
Amesema uwepo wa maelfu ya wananchi waliojitokeza kwenye mkutano huo ni
ushahidi kuwa wilaya hiyo inaendelea kuwa na mazingira ya amani na utulivu,
akibainisha kuwa hali hiyo ikitoweka sekta mbalimbali za uchumi zitaathirika
kwa kiwango kikubwa

Post a Comment