UMMY ATEULIWA MSHAURI WA RAIS AFYA YA UZAZI
RAIS Samia Suluhu Hassan, amemteua Mbunge wa zamani wa Tanga mjini Ummy Mwalimu, kuwa mshauri wake wa masuala ya Afya ya Uzazi, Mama na Mtoto.
Taarifa ya Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Dk Moses Kusiluka iliyotumwa na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais Ikulu jana, ilisema Rais Samia amefanya uteuzi huo.
Ummy, ambaye kitaaluma ni mwanasheria amehudumu katika Baraza la Mawaziri akiwa naibu waziri kwa miaka mitano na waziri kamili kwa miaka tisa tangu mwaka 2010 hadi 2024 ikiwemo Wizara ya Afya kabla ya mabadiliko yaliyofanywa na Rais kumuondoa katika nafasi hiyo mwaka 2024.
Amekuwa mbunge kwa miaka 15, ikiwemo viti maalumu mwaka 2010 na 2015 kabla ya ku jitosa kugombea jimbo la Tanga Mjini mwaka 2020.
Mwaka 2025 hakupata ridhaa ya chama chake (CCM) kupeperusha bendera
katika jimbo hilo baada ya kuengeuliwa katika Kamati Kuu

Post a Comment