SERIKALI YAELEZA SABABU YA UCHUMI IMARA

 


SERIKALI imesema Pato la Taifa kwa mwaka 2025 lilikua kwa wastani wa asilimia 5.9 ikilinganishwa na asilimia 5.5 mwaka 2024.

Waziri wa Fedha, Balozi Khamis Mussa Omar alisema hayo akiwasilisha Mapitio ya Utekelezaji na Mpango wa Bajeti kwa Mwaka wa Fedha 2025/2026 na Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Mwaka wa Fedha 2026/2027 bungeni Dodoma jana.

Balozi Omar alisema ukuaji huo ulichangiwa na kuongezeka kwa mikopo kwa sekta binafsi, kuimarika kwa miundombinu ya usafiri na usafirishaji na kuimarika kwa shughuli za kilimo. Alitaja sababu nyingine ni kutekelezwa kama ulivyopitishwa na bunge.

Kuongezeka kwa uzalishaji wa madini na shughuli za ujenzi wa umma na binafsi na utekelezaji wa miradi ya kimkakati, hususani katika sekta za nishati, usafirishaji na huduma za jamii.

Balozi Omar alisema shughuli za fedha na bima ziliongoza kwa ukuaji wa asilimia 15.7 ikifuatiwa na shughuli za uzalishaji na usambazaji umeme na gesi 11.8%, uchimbaji madini na mawe 9.4%, habari na mawasiliano 8.8%, sanaa na burudani 8.5% na usafirishaji na uhifadhi mizigo 8.0%.

Alieleza kuwa ukusanyaji wa mapato ya kodi umeen delea kuwa zaidi ya asilimia 100 ya lengo la kila mwezi na mpango wa ukopaji kutoka vyanzo vya kibiashara vya ndani na nje kuendelea Alisema hatua za kiutawa la na maboresho ya mifumo ya kielektroniki ya usimamizi wa mapato zimewezesha Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kukusanya mapato ghafi ya Sh trilioni 30.25, sawa na ufanisi wa asilimia 105 ya lengo la kipindi cha rejea.

Alisema mapato halisi yaliyokusanywa na TRA ya likuwa Sh trilioni 29.31 sawa na asilimia 86.0 ya lengo la mwaka na wizara ilikusanya maduhuli ya Sh bilioni 25.5 sawa na ufanisi wa asilimia 47.6 ya lengo la mwaka.

Alisema kati ya Julai 2025 hadi Aprili mwaka huu mapato ya ndani yaliyopati kana ni Sh trilioni 29.34 sawa na ufanisi wa asilimia 85.9 yalengo la mwaka. Balozi Omar alisema kati ya kiasi hicho mapato ya forodha yalikuwa Sh trilioni 11.49, kodi ya mapato Sh trilioni 10.95, kodi ya mlaji Sh trilioni 6.32, mapato yasiyo ya kodi Sh trilioni 1.22 na kodi nyingine Sh bilioni 266.72.

Alisema mwenendo wa viashiria vingine vya uchumi, katika kipindi cha Julai 2025 hadi Aprili mwaka huu una onesha mfumuko wa bei uli kuwa wastani wa asilimia 3.4, ikilinganishwa na wastani wa 3.1% katika kipindi kama hicho mwaka 2024/2025.

“Ongezeko hilo lilito kana na kupungua kwa ugavi wa bidhaa za vyakula katika soko la ndani kufuatia ongezeko la mauzo ka tika masoko ya nchi jirani,” alisema. Balozi Omar alisema akiba ya fedha za kigeni ilikuwa Dola za Marekani milioni 5,722.5, kiasi kinachotosheleza uagizaji wa bidhaa na huduma kutoka nje ya nchi kwa kipindi kisichopungua miezi 4.4.

Alisema pia ilinunua tani 17.64 za dhahabu zenye thamani ya Dola za Marekani milioni 2,616.77 na kufikisha tani 24.21 za akiba ya dha habu zenye thamani ya Dola za Marekani milioni 3,591.39. Aidha, alisema hadi Aprili mwaka huu taasisi zimechan gia Sh bilioni 341.53 katika Mfuko Mkuu wa Hazina ya Serikali sawa na asilimia 79.95 ya lengo la mwaka.

Usimamizi deni Balozi Omar alisema Tanzania imeibuka mshindi wa jumla katika Tuzo ya Usimamizi wa Deni la Umma katika nchi za Jumuiya ya Madola na Tuzo ya Ofisi Bora ya Usimamizi wa Deni la Serikali katika Kanda ya Afrika.

Alisema hadi Aprili mwaka huu Sh trilioni 9.73 sawa na asilimia 68.5 ya lengo la mwaka zimepokele wa na kutumika kulipa deni la serikali lililoiva. Kati ya kiasi hicho, Sh tri lioni 4.44 zimetumika kulipa deni la nje na Sh trilioni 5.29 zimetumika kulipa deni la ndani. “Ufanisi katika ulipaji deni lililoiva umeiwezesha nchi yetu kuendelea kuamini ka katika masoko ya fedha ya kikanda na kimataifa,” alisema.

No comments