TANZANIA IKO TAYARI KWA BIASHARA, UWEKEZAJI NA UBUNIFU


Na Beda Msimbe, TBN, Petersburg, Urusi

Katika hotuba ya kihistoria iliyotolewa kwenye Jukwaa la Kimataifa la Uchumi la St. Petersburg nchini Urusi, Rais wa Tanzania amewahakikishia viongozi wa dunia na wawekezaji wa kimataifa kuwa nchi hiyo iko tayari kwa biashara, uwekezaji mkubwa, na ubunifu wa kisasa ili kuendana na ushindani wa soko la kimataifa. 

Rais Samia akihutubia Jukwaa la Kimataifa la Uchumi la Saint Peterburg, alisema Tanzania imefanya mageuzi makubwa ya kisheria na kitaasisi ikiwemo kuanzisha kituo kimoja cha huduma ambapo usajili wa kampuni sasa huchukua hadi saa 24 tu.

Alisema hatua hiyo imechangia kupaa kwa uwekezaji wa moja kwa moja kutoka nje hadi kufikia dola za Marekani  bilioni 12 mwaka 2025 ikilinganishwa na dola bilioni 3 tu za mwaka 2021.

Ili kuchochea ukuaji huu wa viwanda na biashara, aliwaambia washiriki wa jukwaa hilo kutoka nchi takribani 130, serikali imeweka msisitizo mkubwa katika usindikaji wa madini ya mkakati ndani ya nchi kama vile dhahabu, neli, graphite,na helium badala ya kusafirisha malighafi ghafi.

Aidha alifunguka kuhusu viwanda vya mbolea na kusema kwamba uwekezaji kwenye viwanda vya mbolea kwa kushirikiana na Urusi na kuendeleza miradi mikubwa kama Eneo Maalum la Kiuchumi la Bagamoyo na Bandari ya kimataifa ya Mangapwani kule Zanzibar.

Akizungumzia ujenzi wa uchumi wa kisasa unaoendeshwa na teknolojia na miundombinu madhubuti Rais Samia amesema bado inatafuta washirika katika hilo kwani ni nguzo kuu inayoiweka Tanzania katika nafasi ya kipekee ya kiushindani kuelekea Dira ya Taifa ya Maendeleo ya mwaka 2050 inayolenga kufikia uchumi wa kipato cha kati cha juu wa dola za Marekani trilioni moja.

Akizungumza katika moja ya hotuba zake iliyojaa msisimko katika jukwaa hilo, Rais Samia alibainisha kuwapo kwa mapinduzi makubwa ya miundombinu ikiwemo mtandao wa reli ya kisasa ya SGR inayounganisha Bandari ya Dar es Salaam na nchi jirani, pamoja na mipango ya upanuzi wa reli hadi Musoma na ukanda wa kusini kuelekea Malawi na Msumbiji.

Katika upande wa ubunifu na mawasiliano, alisema Tanzania inakaribisha wawekezaji kwani imekuwa nchi ikovizuri katika mwasiliano ikiwa imefikia asilimia 95 ya upatikanaji wa broadband na inapanua mkongo wa taifa wa mawasiliano ili kuwa kitovu cha kidijiti kwa nchi saba zisizo na bahari. 

Aidha, akizunguzmai mustakabali wa nishati, Rais alitangaza mpango wa taifa wa nishati ya nyuklia kwa matumizi ya amani kupitia teknolojia ya vinu vidogo kwa kushirikiana na kampuni ya Rostam ili kukidhi mahitaji ya megawati 80,000 ifikapo mwaka 2030, jambo linalothibitisha utayari wa Tanzania kuongoza mabadiliko ya kiuchumi Afrika.

@@@@@@@@@@@@@@

No comments