PUTIN AIKUBALI TANZANIA AELEZA JINSI ILIVYO MUHIMU




Na Beda Msimbe, TBN, Petersburg

Rais Vladimir Putin wa Urusi amesema Tanzania ni lango kuu la kimkakati linalounganisha soko la Afrika Mashariki na masoko ya kimataifa.

Aidha amesema katika uchumi wa dunia unaozidi kubadilika kuelekea mifumo ya nguzo nyingi za kiuchumi, taifa la Tanzania umuhimu  mkubwa katika kuyfanikisha ustgawi wa jamii mbalimbalio. 

Akizungumza Juni 5 katika Jukwaa la Kimataifa la Uchumi la St. Petersburg la mwaka 2026 Rais Putin amesema kuwa Tanzania katika utendaji ni taifa la kimkakati  katika Ukanda wa Afrika Mashariki unaofanana na ule wa nchi ya Uzbekistan katika ukanda wa Asia ya Kati ikifanya kazi kama kiungo muhimu sana kati ya uchumi wa kikanda na vituo vikuu vya biashara ya kimataifa duniani. 

Kiongozi huyo amebainisha hayo wakati akizungumzia mataifa ambayo kutokana na nafasi zao za kijiografia na mahusiano yao ya kiuchumi yanageuka kuwa madaraja muhimu kati ya kanda tofauti duniani na kuongeza kuwa mataifa yenye uwezo wa kuoanisha maendeleo yao ya ndani na miunganisho madhubuti kwenye vituo vipya vya ukuaji wa uchumi wa kimataifa yanazidi kuwa muhimu wakati mifumo ya biashara ya kimataifa inavyoendelea kubadilika.

Kauli hizi nzito kutoka kwa Rais Putin zinakuja wakati ambao Tanzania inaendelea kupanua kwa kasi miundombinu yake ya usafirishaji ikiwemo bandari na njia za biashara za kikanda ili kuimarisha nafasi yake kama kitovu kikuu cha biashara kwa ukanda mzima wa Afrika Mashariki na Kati na hivyo kutafsiri kwa vitendo malengo makubwa ya ukuaji wa kiuchumi.

Rais Samia Suluhu Hassana alishiriki katika jukwaa hilo amnbapo alipata nafasi ya kuelezea mambo mbalimbali yanayohusiana na uwekezaji na pia biashara.

Aidha alisema Tanzania ipo tayari kushirikiana na mataifa yoyote ikiwamo Urusi ili kupeleka fursa mbalimbali za maendeleo kwa wananchi wake.Akijibu swali kwamba Russia ina vikwazo, Rais Samia alisema Tanzania haina vikwazo inafanyakazi na washirika wote wanaoitakia mema nchi yake

No comments