BUNGE LATAJA MAENEO 13 KUIMARISHA UCHUMI


KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti imetaja maeneo 13 ambayo serikali inapaswa kuyafanyia kazi kwa haraka, kuimarisha usimamizi wa fedha za umma, kuongeza ufanisi wa taasisi za kifedha na kuimarisha uchumi wa nchi.

Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Bajeti, Mashimba Ndaki ameyasema hayo akiwasilisha maoni na mapendekezo ya kamati hiyo kuhusu Makadirio na Matumizi ya Bajeti ya Wizara ya Fedha kwa Mwaka wa Fedha 2026/2027.

Ndaki alisema katika eneo la Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi, kamati hiyo ilibainisha kuwa pamoja na deni la serikali kuwa himilivu, uwiano wa deni kwa mauzo ya nje ume fikia asilimia 13.9 dhidi ya ukomo wa asilimia 15.

Kutokana na hali hiyo, alisema wameshauri serikali kuongeza uwekezaji katika sekta zinazochochea mauzo ya nje, kupunguza ukopaji wa ndani na kuimarisha thamani ya Shilingi.

Aidha, kamati hiyo imeeleza wasiwasi wake kuhusu muundo wa Idara ya Mkaguzi Mkuu wa Ndani wa Serikali, ikitaka kufanyika marekebisho ya kimuundo na kutungwa kwa Sheria ya Ukaguzi wa Ndani ya Umma kuongeza uwajibikaji na uhuru wa wakaguzi wa ndani.

Miongoni mwa maeneo mengine aliyoyataja ni uteuzi wa makamishna wa Tume ya Pamoja ya Fedha ambao haujafanyika kwa miaka saba, kukamilishwa kwa jengo la tume ifikapo Septemba 2026, na kuondoa matumizi yasiyo na tija katika mafungu ya serikali.

Ndaki alisema pia wa naitaka Hazina kusimamia kwa karibu matumizi ya fedha za umma, kudhibiti ongezeko la madeni ya waz abuni, kuhakikisha manunuzi yanafanyika kwa bei stahiki na kuimarisha matumizi ya mfumo wa NeST.

Aidha, aliitaka serikali kufuatilia kwa karibu hoja za ukaguzi ambazo asilimia 67 hazijapatiwa majibu, hali inayochangia kujirudia kwa dosari katika matumizi ya fedha za umma.

Katika usimamizi wa mifuko maalumu, alisema kamati imependekeza mapato yanayokusanywa na Mamla ka ya Mapato Tanzania (TRA) kutoka vyanzo maalumu yawasilishwe moja kwa moja kwenye mifuko husika kuondoa changamoto za ukwasi na ucheleweshaji wa miradi.

Mapendekezo mengine yanahusu kuimarisha usi mamizi wa vihatarishi vya bajeti, kuongeza fedha kwa Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi, kuanzisha sera ya benki za maende leo, kuandaa sera mahsusi ya ufadhili wa sekta ya kilimo, kuimarisha utekelezaji wa miradi ya ubia kati ya sekta ya umma na binafsi (PPP), kufungua masoko ya mitaji kwa tahadhari pamoja na kurejesha mamlaka kamili kwa TRA kuajiri na kuchukua hatua za kinidhamu kwa watumishi wake.

 

Ndaki alisema utekelezaji wa mapendekezo hayo utasaidia kuimarisha nidhamu ya fedha, kuongeza ufanisi wa taasisi za umma na kuweka msingi imara wa kufikia malengo ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050.

No comments