RAIS SAMIA KUMALIZA ZIARA YAKE URUSI LEO
Na Beda Msimbe,
TBN, St Petersburg
Rais Samia
Suluhu Hassan leo anahitimisha ziara yake nchini Urusi kwa kushiriki katika
kongamano la kibiashara kati ya Tanzania na Urusi sanjari na Jukwaa la Kimataifa
la Biashara la St Petersburg.
Katika jukwaa
hilo Rais Samia anatarajiwa kuinadi Tanzania katika sekta za uwekezaji na
biashara.
Ziara ya Rais Samia
imekuwa na mafanikio makubwa hasa hakikisho la ushiriano wa karibu na Urusi
katika nyanja mbalimbali ikiwemo elimu ya uendelezaji wa rasilimaliwatu na
ukuzaji wa teknolojia.
Ziara hiyo
katika taifa lenye nguvu kubwa kiteknolojia, uchakataji na uzalishaji kwenye
kilimo au viwandani imekuja wakati Tanzania inajiandaa kutekeleza Dira ya Taifa
ya Maendeleo ya 2050 inayolenga kulifanya taifa kuwa na pato la dola trilioni
moja kwa mwaka.
Kwa sasa serikali
imesema Pato la Taifa kwa mwaka 2025 lilikua kwa wastani wa asilimia 5.9
ikilinganishwa na asilimia 5.5 mwaka 2024 kauli ilitolewa na Waziri wa Fedha,
Balozi Khamis Mussa Omar wakati akiwasilisha Mapitio ya Utekelezaji na Mpango
wa Bajeti kwa Mwaka wa Fedha 2025/2026 na Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa
Mwaka wa Fedha 2026/2027 bungeni Dodoma hivi karibuni.
Balozi Omar
alisema ukuaji huo ulichangiwa na kuongezeka kwa mikopo kwa sekta binafsi,
kuimarika kwa miundombinu ya usafiri na usafirishaji na kuimarika kwa shughuli
za kilimo.
Alitaja sababu
nyingine ni kuongezeka kwa uzalishaji wa madini na shughuli za ujenzi wa umma
na binafsi na utekelezaji wa miradi ya kimkakati, hususani katika sekta za
nishati, usafirishaji na huduma za jamii.
Mwisho Mwisho
mwisho

Post a Comment