Mchungaji
Richard Hananja amewataka vijana kutafakari kwa kina kabla ya kushiriki katika
vitendo vinavyoweza kuhatarisha amani na utulivu wa nchi, akisisitiza kuwa
tofauti za mitazamo zinapaswa kuwa chachu ya mazungumzo na maelewano badala ya
kusababisha migawanyiko katika jamii.
Akizungumza
na waandishi wa habari jijini Dodoma, Hananja amesema matumizi yasiyo sahihi ya
mitandao ya kijamii yanaweza kuchochea chuki, matusi na vurugu, hali inayoweza
kuathiri mshikamano wa kitaifa.
Amehimiza
vijana kutumia majukwaa ya kidijitali kwa uwajibikaji, kuheshimu maoni ya
wengine na kuendeleza maadili yanayojenga umoja, amani na maendeleo ya jamii.
Hananja
amesisitiza kuwa vijana wana nafasi muhimu katika kulinda amani ya taifa na
kwamba ushiriki wao katika mijadala ya kijamii na kisiasa unapaswa kuongozwa na
busara, heshima na uzalendo.
Post a Comment