'HAKUNA HAJA YA KUANDAMANA SERIKALI ITAWAPA KATIBA MPYA'
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na uwekezaji Prof. Kitila Alexander Mkumbo amesisitiza kwamba Tanzania inatawaliwa na kuongozwa na misingi ya kidemokrasia na utawala wa sheria na utawala bora, akibainisha kwamba serikali ya Chama Cha Mapinduzi CCM inaenda kutekeleza ahadi yake ya kupatikana kwa Katiba mpya kama ilivyoahidi katika Ilani ya CCM ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzannia wa Mwaka 2025.
Waziri Kitila Mkumbo amebainisha hayo bungeni jijini Dodoma wakati akihitimisha mjadala wa taarifa ya uchumi na mpango wa Taifa wa maendeleo, akiwakosoa wale wanaoitisha maandamano na kueleza kuwa hakuna chama kingine chenye ajenda ya kupatikana kwa Katiba mpya nje ya chama tawala kinachounda serikali.

Post a Comment