Dk. Kikwete yuko Juba akisaka suluhu Sudan Kusini
Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Jakaya Mrisho Kikwete ameendelea kupeperusha vyema bendera ya nchi na Umoja wa Afrika (AU) kufuatia mfululizo wa vikao vya kimkakati vilivyolenga kusaka amani ya kudumu nchini Sudan Kusini.
Katika ziara hiyo ya kidiplomasia mjini Juba, Dk. Kikwete amefanya mazungumzo mazito na Rais wa nchi hiyo, Salva Kiir Mayardit, kabla ya kukutana na kufanya majadiliano na viongozi wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama, pamoja na mabalozi wa mataifa ya Afrika wanaowakilisha nchi zao nchini humo ili kuweka misingi imara ya utulivu wa kikanda.
![]() |
| Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika kikao na Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama vya Sudani Kusini. |
![]() |
| Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika majadiliano na Mabalozi wa nchi za Afrika wanaowakilisha nchi zao Sudani Kusini |
![]() |
| Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete baada ya kumaliza Mkutano wake na Rais Salva Kiir Mayardit wa Sudani Kusini |
![]() |
| Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje wa Sudan, Balozi Dkt. James Pitia Morgan (wa kwanza kulia), Waziri wa Masuala ya Ofisi ya Rais, Africano Mande Gedima (kushoto kwake) na Mwakilishi wa Umoja wa Afrika nchini Sudani Kusini, Abdiweli Ali Mohamed Gaas. Wengine katika picha ni timu ya wataalamu kutoka Tanzania na Umoja wa Afrika wanaomsaidia Dkt. Jakaya Kikwete katika jukumu hilo. |
Vikao hivi vimezidi kuongeza imani ya kikanda kwa Tanzania kama taifa nguzo katika usuluhishi wa migogoro barani Afrika.
Katika ziara hiyo Dk Kikwete aliambatana na jopo la wataalamu wa masuala mbalimbali ya kiutawala.
Katika kilele cha ziara hiyo Dk. Kikwete alihutubia Jukwaa la Pili la Ushirikiano wa Umajumui wa Afrika lililoandaliwa na Serikali ya Sudan Kusini.
Katika jukwaa hilo, kiongozi huyo mkongwe aliongoza mjadala mkali wa namna bora ya kutafuta suluhu ya changamoto zinazoikabili nchi hiyo, akisisitiza dhana ya kupata "suluhisho la Kiafrika kwa matatizo ya Afrika" kama njia pekee na salama ya kuleta ustawi na amani ya kudumu kwa wananchi wa Sudan Kusini.





Post a Comment