Samia aweka shada kaburi la askari asiyefahamika
Na Beda Msimbe, TBN,Moscow
KENGELE kubwa iliyogongwa mara tisa, bendi ya jeshi ikiongoza nyimbo za maombolezo Rais Samia Suluhu Hasan majira ya saa tano na dakika 23 aliweka shada la maua kwa kaburi la askari asiyefahamika, mjini Moscow.
Aidha baada ya shughuli la uwekaji wa taji hilo katika eneo ambalo moto huwaka daima ikiwa ni kumbukumbu ya wapiganaji wa Urusi waliopoteza maisha katika vita kuu ya pili, gadi tatu zilipita kwa mwendo wa haraka na kutoa heshima kwa Rais Samia baada ya kupigwa kwa wimbo wa taifa la Tanzania.
Hali ya askari katika uwanja huo walioonesha nidhamu ya hali ya juu ya kusimama tisti katika maeneo yao bila kutikisika , ubadilishanaji wa gadi za ulinzi na pia mwendo wa pole ambao ulimsindikiza Rais Samia kwenda kwenye tukio la uwekeaji wa shahada. Vilikuwa vitu vinavyovutia kuangalia.
Rais Samia ambaye yupo katika ziara ya kiserikali baadaye alikwenda kukutana na mwenyeji wake Rais Vladmir Putin .
Zaidi ya maofisa 300 wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania JWTZ wamepata nafasi ya masomo katika nchi ya Urusi kwa ajili ya shahada ya kwanza na ya pili.
Askari hao wameenda kujifunza masuala ya kupambana na ugaidi, sayansi na teknolojia,mafunzo ya kijeshi, ulinzi wa amani, ununuzi na uhifadhi wa silaha,namna ya kukabiliana na majanga.
Tanzania na Urusi zina ushirikiano wa kijeshi kwa kuzingatia makubaliano ya ushirikiano wa kijeshi yaliyosainiwa mwaka 2016 na makubaliano ya mwaka 2018 ya ushirikiano wa kifundi wa kijeshi.
Tanzania yenye ukuaji wa uchumi wa asilimia 5.5 kwa mwaka 2024 na ikikadiriwa kufikia asilimia 6 mwaka huu na ikiwa na mkakati wa kuhakikisha kwamba Dira ya maendeleo ya mwaka2050 inatekelezwa ziara ya Rais Samia nchini Urusi inatarajiwa kuzaa matunda yanayotarajiwa ya kuinua sekta ya ajira kukuza biashara na kuimarisha uwekezaji.
.jpg)


Post a Comment