UPANUZI WA BANDARI YA DAR ES SALAAM: GATI 10 MPYA NA MIUNDOMBINU YA UBARIDI KUWEZESHA USAFIRISHAJI WA MAZAO YA MBOGAMBOGA



Msemaji Mkuu wa Serikali Gerson Msigwa ,  amesema Serikali imeanza utekelezaji wa mradi mkubwa wa upanuzi wa Bandari ya Dar es Salaam utakaogharimu dola za Marekani bilioni 2, sawa na zaidi ya shilingi trilioni 5.

Amesema moja ya lengo la upanuzi huo ni kutatua changamoto za usafirishaji wa mazao ya kilimo yanayoharibika haraka.

Akizungumza na waandishi wa habari mkoani hapa alisema Mradi huo unahusisha ujenzi wa gati mpya 10 ili kufikisha jumla ya gati 22.

Aidha kutakuwepo na ujenzi wa majengo ya ubaridi na miundombinu yake maalumu ili kuondoa vikwazo vilivyokuwa vikiwakabili wakulima wa parachichi na mbogamboga wakati wa kusafirisha bidhaa zao nje ya nchi.

Kupitia mradi huu, Serikali pia itaboresha barabara za kuingia na kutoka bandarini kwa kujenga barabara za mzunguko ili kupunguza msongamano wa magari yanayobeba mizigo, jambo litakalosaidia mazao kutoka mikoa ya uzalishaji kama Njombe kufika bandarini kwa wakati na yakiwa na ubora uleule.

No comments