HIFADHI YA MPANGA KIPENGERE KUWANIA TUZO ZA KIMATAIFA ZA MWAKA 2026
Sekta ya
utalii mkoani Njombe inapata msukumo mpya ambapo Hifadhi ya Pori la Akiba la
Mpanga Kipengere imeingia kwenye mchuano wa kuwania tuzo za dunia (World
Tourism Awards) katika vipengele vya sehemu bora ya fungate barani Afrika na
sehemu bora ya utalii
Hifadhi
hii yenye ukubwa wa kilomita za mraba 1,400 ina utajiri wa maporomoko ya maji
yapatayo 50, bustani za asili za maua ya orchid, na maeneo ya kihistoria kama
pango la Mtemi Mkwawa, jambo linalofanya eneo hili kuwa kivutio adhimu kwa
watalii wa ndani na nje
Msemaji Mkuu wa Serikali Gerson Msigwa alisema
hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu ufanisi wa miradi ya
kimkakati iliyopo mkoani Njombe.
Alisema Serikali
inaendelea kuimarisha miundombinu katika hifadhi hiyo pamoja na Hifadhi ya
Taifa ya Kituro inayojulikana kama 'Bustani ya Mungu', huku ujenzi wa hoteli na
kambi za watalii ukihamasishwa ili kuongeza idadi ya vitanda na kujiandaa tayari
kwa michuano ya AFCON 2027 ambapo Tanzania itakuwa mwenyeji

Post a Comment