MAFAO YA PENSHENI NA MATIBABU SASA KUWAFIKIA BODABODA, WAKULIMA NA MAMA LISHE
Serikali ya
Awamu ya Sita imezindua mfumo wa 'Hifadhi Skimu' kupitia Mfuko wa Taifa wa
Hifadhi ya Jamii (NSSF) uliolenga kuleta mageuzi katika mfumo wa hifadhi ya
jamii kwa kuwajumuisha wananchi waliojiajiri katika mfumo rasmi wa kujiwekea
akiba
Mpango huo
unatekelezwa chini ya miongozo ya Dira ya Maendeleo ya Taifa ya 2050, ukilenga
kuwafikia mamilioni ya Watanzania wakiwemo wakulima, wafugaji, wavuvi,
wachimbaji wadogo wa madini, pamoja na wajasiriamali wadogo kama waendesha
bodaboda na mama lishe
Kupitia Hifadhi Skimu, wananchi sasa watakuwa na uhakika wa maisha ya sasa na ya baadaye kwa kunufaika na mafao mbalimbali yakiwemo pensheni ya uzee, urithi, ulemavu, uzazi, na huduma za matibabu kupitia michango yao ya hiari
Msemaji wa serikali Gerson Msigwa akihimiza wananchi
wajiunge na mfumo huo alisema kwamba ni rahisi kwani NSSF imeweka mfumo rahisi
wa kujiandikisha na kuchangia kwa kutumia simu ya kiganjani kwa kupiga namba ya
huduma 15200# na kufuata
maelekezo rahisi
Hatua hii
inalenga kuondoa dhana ya zamani kuwa hifadhi ya jamii ni kwa ajili ya
watumishi wa sekta rasmi pekee, na badala yake kuwapa kinga ya kijamii wananchi
wote wanaojituma katika kazi mbalimbali za uzalishaji mali

Post a Comment