THAMANI YA MAKAA YA MAWE YAFIKIA TRILIONI MOJA: TANZANIA KUWA KITOVU CHA NISHATI AFRIKA MASHARIKI NA KATI
Tanzania
inaelekea kuwa kitovu cha uzalishaji wa nishati kupitia makaa ya mawe ambapo
thamani ya madini hayo yaliyochimbwa imeongezeka kwa kasi kutoka shilingi
bilioni 228.8 katika mwaka wa fedha 2020/21 hadi kufikia takribani shilingi
trilioni moja mwaka 2022/23
Uzalishaji
umeongezeka kutoka tani 744,923 hadi kufikia tani 3,007,180 kwa mwaka, huku
nchi ikiwa na akiba iliyothibitishwa ya takribani tani bilioni 5 katika mikoa
ya Ruvuma, Songwe, Rukwa, na Njombe
Kupitia msemaji wake Gerson Msigwa,
Serikali imesema imejipanga kuboresha miundombinu ya
barabara kuelekea migodini na kukuza soko la ndani ili makaa hayo yatumike
zaidi katika kuzalisha vyuma, saruji, na nishati ya majumbani, hali
itakayopunguza gharama za uzalishaji na kuongeza ushindani wa bidhaa za
Tanzania katika masoko ya nje
Wakati huo huo kuna mapinduzi mikubwa ya miundombinu katika mkoa wa Njombe. Imeelezwa katika mkutano na waandishi wa habari na msemaji wa serikali Geson Msigwa kuwa bajeti ya Tarura imeongezeka kwa asilimia 149 kwa lengo la kufungua barabara za mashambani.
Alisema Serikali
ya Awamu ya Sita imeleta mageuzi makubwa ya miundombinu ya barabara mkoani
Njombe kwa kuongeza bajeti ya TARURA kutoka wastani wa shilingi bilioni 8.44
hadi kufikia bilioni 21.07 kwa kipindi cha mwaka 2021-2026, ambalo ni ongezeko
la asilimia 149.64
Amesema ongezeko
hilo limesaidia kuongeza mtandao wa barabara za lami kutoka kilometa 38.7 hadi
kilometa 95.5, huku barabara za changarawe zikiongezeka na kufikia kilomita
2,097.40, jambo lililosaidia kufungua barabara mpya maeneo ya kilimo cha
parachichi, chai, na viazi
Aidha,
ujenzi wa madaraja umeongezeka kutoka 352 hadi 386 na kalvati kufikia 2,962,
hatua inayohakikisha kuwa asilimia 70 ya mtandao wa barabara mkoani humo
unapitika katika majira yote ya mwaka, hivyo kurahisisha huduma za kijamii na
kusafirisha mazao kwenda sokoni

Post a Comment