RAIS SAMIA APOKEA UJUMBE WA JUMUIYA YA MADOLA IKULU, DAR ES SALAAM
Katibu
Mkuu wa Jumuiya ya Madola, Bi. Shirley Ayorkor Botchwey. amesisitiza dhamira ya
Jumuiya ya Madola kuendelea kushirikiana na Tanzania katika kuimarisha misingi
ya demokrasia, utawala bora na maridhiano ya kitaifa.
Aidha
amesema kuwa Jumuiya hiyo inaunga mkono juhudi zinazoendelea nchini na iko
tayari kusaidia kujenga mazingira ya kisiasa yenye utulivu, ushirikishwaji na
kuaminiana kupitia mazungumzo na mageuzi ya taasisi.
Hayo
yamo katika ujumbe wake uliowasilishwa na Mjumbe Maalum na Rais Mstaafu wa
Jamhuri ya Malawi, Mhe. Dkt. Lazarus McCarthy Chakwera kwa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, katika Ikulu ya Dar es
Salaam, leo.
Jumuiya
ya Madola imesema kwamba inafuatilia kwa makini matukio yaliyojitokeza wakati
na baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025, ikiktaka kushiriki kwa uwazi katika
juhudi za kuendeleza majadiliano ya vyama na kuimarisha uwajibikaji wa taasisi.
Akizungumza
wakati wa kupokea ujumbe huo, Rais Dkt. Samia amesema Tanzania inaendelea
kushughulikia hali hiyo kupitia taasisi zake, akizitaja hatua zilizochukuliwa
na Serikali ikiwemo kuunda Tume Huru ya Uchunguzi kwa lengo la kurejesha
utulivu na kuimarisha uwajibikaji.
Amebainisha
kuwa matokeo ya Tume hiyo yataongoza hatua zinazofuata ikiwemo uwajibikaji,
maridhiano na mageuzi ya taasisi, huku Serikali ikiendelea kusimamia mchakato
wa maridhiano kupitia majukwaa ya kisheria na ushirikishwaji wa wadau
mbalimbali.
Kwa
upande wake, Mhe. Chakwera ameeleza utayari wa Jumuiya ya Madola kuendelea
kushirikiana na Tanzania katika kuimarisha utawala wa sheria na mshikamano wa
kitaifa.
Dkt.
Chakwera amehitimisha ziara yake ya kikazi nchini baada ya kufanya tathmini ya
hali ya kisiasa na kufanya mazungumzo na wadau mbalimbali wa kisiasa na
kitaasisi nchini.
.jpeg)
.jpeg)
Post a Comment