TANZANIA NI JIBU: BANDARI YA DAR ES SALAAM YAZIBA MIDOMO WABABAISHAJI NA WAZUSHI



Wakati mataifa jirani yakipata pumzi ya kiuchumi kupitia lango kuu la Afrika Mashariki na Kati, Bandari ya Dar es Salaam, kelele za wababaishaji wanaoitafutia Tanzania maangamizi kwa propaganda za uongo zimeendelea kuzamishwa na ukweli wa takwimu na utendaji uliotukuka. 

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imedhihirisha kuwa si tu nguzo ya diplomasia, bali ni mhimili wa uhai wa kiuchumi kwa nchi zisizo na bandari, ikiongoza mapinduzi ya upatikanaji wa nishati ya mafuta kwa uhakika na kasi inayowaacha wapinzani wa maendeleo bila majibu.

Ukweli huu usiohitaji tochi umethibitika  Machi 24, 2026, wakati wa ziara ya Waziri wa Nishati na Madini wa Malawi, Dkt. Jean Mathanga, alipokagua miundombinu ya mafuta katika Kituo cha Kurasini Oil Jet (KOJ-1). 

Katika hali inayowapa somo wazushi wote, Dkt. Mathanga ameishukuru Serikali ya Tanzania kwa uungwana na uwezo wake wa kuituliza Malawi dhidi ya tishio la uhaba wa mafuta, akisisitiza kuwa bila miundombinu imara ya Tanzania, shughuli za kiuchumi na maisha ya wananchi wa Malawi yangekuwa shakani. Hii ni sifa ya kipekee kwa Tanzania ambayo imekuwa ikitumia rasilimali zake si kwa kujinufaisha pekee, bali kwa kuleta ustawi wa kikanda.

Kufunguka kwa lango la Tanzania kwa nchi ya Malawi si bahati mbaya, bali ni matokeo ya uwekezaji mkubwa na usimamizi makini wa Mfumo wa Uagizaji Mafuta kwa Pamoja (BPS). 

Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Petroli kutoka PBPA, Mhandisi Bruno Tarimo, amefafanua kwa ujasiri kuwa sehemu kubwa ya mafuta yanayoingia Malawi sasa yanapita Tanzania kwa usalama na ufanisi wa hali ya juu. Mafanikio haya ni jibu tosha kwa wale wanaodai kwa uongo kuwa Tanzania inapoteza ushindani, kwani ukweli unaonesha nchi jirani zinazidi kuongeza imani na kutegemea miundombinu yetu kwa mahitaji yao ya kimkakati.

Msisitizo unabaki kuwa Tanzania chini ya uongozi huu madhubuti, haitayumbishwa na narashi za uongo zinazopikwa na watu wasiolitakia mema taifa. 

Bandari ya Dar es Salaam itaendelea kuwa kielelezo cha ufanisi, ikichochea uchumi wa Malawi na mataifa mengine, huku ikiwaacha wababaishaji wakijitafuna kwa husuda. Huu ndio msimamo wa nchi inayojua thamani yake, inayolinda heshima yake, na inayohakikisha kuwa ukweli wa mafanikio unazungumza kwa sauti kuu kuliko kelele za wapashaji habari za uzushi.

No comments