Makonda: Tumieni fursa ya AFCON kuonesha vipaji vya michezo mingine

 



WAZIRI wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Paul Makonda amewataka viongozi wa mashirikisho ya michezo kutumia fursa ya mashindano makubwa ya soka barani Afrika kuitangaza Tanzania na kuonesha vipaji vya michezo mingine.

Makonda amesema maandalizi ya mashindano hayo yanapaswa kuwa fursa kwa michezo yote nchini, siyo soka pekee.

Akizungumza kwenye mkutano wa Baraz,,a la Michezo la Taifa  (BMT) uliofanyika katika Uwanja wa Benjamin Mkapa Machi 13,2026 , amesema ujio wa wageni wengi nchini   kutumiwa kutangaza vipaji vya wanamichezo wa Tanzania.


“Hii ni nafasi ya kuonesha dunia vipaji tulivyonavyo. Si kila anayependa michezo ni wa soka pekee, kuna wengine wanapenda ngumi, tenisi, riadha na michezo mingine,” amesema.

Amesisitiza kuwa mashirikisho yanapaswa kuandaa matukio na maonesho ya michezo ili kuitangaza Tanzania kimataifa na kuvutia uwekezaji kwenye sekta hiyo.





No comments