SAMUEL ETO’O AWASILI TANZANIA KUSHIRIKI MKUTANO WA KAMATI YA UTENDAJI YA CAF
Mwanasoka nguli wa zamani ambaye pia ni Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Cameroon, Samuel Eto’o, amewasili nchini leo, Februari 12, 2026, katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwl. Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam.
Eto’o ni miongoni mwa wajumbe wa Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF), watakaoshiriki Mkutano wa kamati ya utendaji ya CAF utakaofanyika kesho, Februari 13, 2026, jijini Dar es Salaam.
Ujio wake pamoja na viongozi wengine wa juu wa soka barani Afrika unaendelea kuipa Tanzania heshima kubwa kama mwenyeji wa mkutano huo muhimu wa kimataifa, unaolenga kujadili na kuimarisha maendeleo ya mpira wa miguu barani Afrika.
Post a Comment