RAIS SAMIA AANZA ZIARA YA KITAIFA URUSI





Na Beda Msimbe, TBN,Moscow
Rais Samia Suluhu Hassan amewasili katika Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa wa Vnukovo, jijini Moscow kwa ajili ya ziara ya kitaifa, nchini Urusi.

Katika ziara hiyo ya kihistoria ikifanywa kwa mara ya pili katika historia ya uhusiano wa Tanzania na Urusi, ya kwanza ilikuwa ni miaka ya 1960 iliyofanywa na Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere, Rais Samia anaendeleza kampeni kubwa ya kuhakikisha Tanzania inanufaika pia kichumi na uhusiano mzuri na mataifa mbalimbali.

 

Kwa mujibu wa shughuli atakazofanya Rais Samia akiwa Urusi kwa lengo la kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia, kisiasa, kiuchumi na kihistoria baina ya Tanzania na Urusi, Rais amekuja kuiweka Tanzania katika ramani ya uwekezaji na pia kutengeneza raslimali watu ambayo taifa inahitaji katika kufanuisha utekelezaji wa Dira ya Maendeleo ya Taifa ya 2050.

 

Alipowasili  majira ya saa 2:25, japo jua bado lilikuwa linawaka,  Rais Samia Suluhu Hassan alipokea heshima ya wimbo wa Taifa pamoja na gwaride.

 

Rais Samia alipokewa na Waziri wa Maendeleo ya Uchumi wa Shirikisho la Urusi, Maxim Reshetnikov.

Kwa mujibu wa ratiba leo asubuhi ataanza na kuweka shada ka maua kwa kaburila askari asiyejulikana kabla ya kwenda Ikulu ya Kremlin kwa mazungumzo.



No comments