KOMPYUTA YATABIRI MSIBA KWA SENEGAL FAINALI ZA AFCON 2025



Kompyuta imetoa utabiri wake kuelekea mchezo wa fainali ya Mataifa ya Afrika (AFCON 2025) unaopigwa Jumapili  Januari 18 nchini Morocco, ikitabiri kifo kwa Senegal na kuibeba Morocco.

Huku kila timu ikisaka taji la pili la bara hili baada ya Morocco kubeba mara ya mwisho mwaka 1978 na Senegal  mwaka 2021, Senegal, komyuita hiyo ambayo pia ilitabiri timu zilizofuzu fainali baada ya vigogo kama Misri na Nigeria kutupwa nje ya mashindano, imesema kombe linaenda Morocco.

Komyuta hiyo inayomilikiwa na Kampuni ya Opta, kupitia mifumo yake ya kisasa imetoa tathmini ya mwisho kuelekea pambano hilo linalosubiriwa kwa hamu kubwa litakalopigwa katika dimba la Prince Moulay Abdellah jijini Rabat. 

Huku Mataifa haya mawili yakikutana yakiwa na rekodi ya kuwa na taji moja kila mmoja, presha kubwa ipo kwa wenyeji Morocco ambao wanatakiwa kutumia vyema uwanja wa nyumbani. Baada ya kufika nusu fainali ya Kombe la Dunia mwaka 2022, macho yote ya mashabiki yatakuwa kwa vijana wa kocha Walid Regragui kuona kama wataweza kurejesha heshima iliyopotea tangu miaka ya sabini.

Katika safari yao kuelekea hatua hii, timu zote mbili zimekuwa na mienendo thabiti ambapo Senegal waliiondosha Misri kwa bao la Sadio Mane, huku Morocco wakihitaji mikwaju ya penalti kuwatoa Nigeria. Kwa mujibu wa Opta, Morocco wanapewa asilimia 54.57 ya kutwaa ubingwa huo kutokana na faida ya nyumbani na ubora wa kikosi chao. Hii ina maana kuwa Senegal wanapewa nafasi ya asilimia 45.43 ya kuwavua nguo Simba wa Milima ya Atlas mbele ya mashabiki wao.

Kocha wa Senegal, Pape Thiaw, amekiri kuwa Morocco ndio wanaopewa nafasi kubwa kutokana na ubora wao katika viwango vya FIFA ambapo wanakamata nafasi ya kwanza barani Afrika na ya 11 duniani. 

Safari ya Morocco ilianzia kwa ushindi dhidi ya Comoro, sare na Mali na kuichapa Zambia katika hatua ya makundi kabla ya kuwatoa Tanzania, Cameroon na hatimaye Nigeria. Kwa upande wao, Senegal walizifumua Botswana na Benin, wakatoka sare na DR Congo kisha wakazivua kofia Sudan na Mali kuelekea hatua hii ya mwisho.

Mbali na taji, macho yatakuwa kwa mastaa Brahim Diaz wa Morocco na Sadio Mane wa Senegal ambao wanawania tuzo ya mchezaji bora wa mashindano. Diaz anaongoza kwa mabao matano akisaka kiatu cha dhahabu, huku Mane akiwa na mabao mawili na pasi tatu za mabao. Hata hivyo, Senegal wataingia vitani wakiwa na pigo baada ya nahodha wao Kalidou Koulibaly na Habib Diarra kufungiwa mchezo huo kutokana na kuwa na kadi mbili za njano walizopata katika hatua za mtoano.

No comments