Max Verstappen Aibuka Kidedea Katika Mbio za langalanga Singapore
![]() |
| Russel akitoka katika gari baada ya ajali |
Dereva
wa timu ya Red Bull Max Verstappen ameibuka kidedea katika mbio za langalanga (F1)
za Singapore Grand Prix zilizogubikwa na matukio mengi ya kusisimua baada ya
dereva wa Mercedes, George Russell kupata ajali akiwa anaongoza mbio hizo.
Mvua kubwa ilisababisha
mbio hizo kuchelewa kuanza kwa dakika 30 huku nusu ya uwanja ukiwa mkavu na
nusu nyingine ikiwa na maji mengi.
Russell aliyekuwa
anaongoza alifanya kosa dogo kwenye kona ya mwisho ya mzunguko wa kwanza baada
ya kushika mstari mweupe na kupoteza uelekeo wa gari lake ambalo liligonga
ukuta wa ndani na kurudi uwanjani huku magari mengine yakimkwepa kwa miujiza.
Ushindi
huo unakuwa wa pili kwa Verstappen ndani ya siku saba kufuatia ushindi wake wa
kwanza msimu huu nchini Malaysia na ni mara yake ya kwanza kuibuka mshindi
katika mzunguko wa Singapore.
Nyuma ya
Verstappen alikuwepo dereva wa Ferrari Lewis Hamilton aliyepanda hadi nafasi ya
pili baada ya kuanza kwa kasi kubwa kutoka nafasi ya sita akifuatiwa na mtu wa
timu yake, Charles Leclerc aliyehitimisha jukwaa la washindi watatu wa kwanza.
Verstappen
alimudu presha kutoka kwa Hamilton mara baada ya gari la usalama kuondoka
uwanjani na hatimaye kuongeza mwendo na kuibuka mshindi kwa utulivu mkubwa.
Mzunguko
wa mwisho wa mbio hizo ulishuhudia drama kubwa baada ya madereva wa McLaren,
Lando Norris na Oscar Piastri kugongana wakati Norris alipojaribu kumpita
mwenzake kwenye kona ya tano.
Ajali hiyo
ilimfanya Piastri kujiondoa mbioni baada ya kugonga kizuizi. Mgongano huo
ulimpa faida kubwa dereva wa Mercedes Kimi Antonelli aliyepanda hadi nafasi ya
nne na kuongeza uongozi wake wa msimamo wa ubingwa wa dunia hadi pointi 89 huku
nafasi za tano hadi saba zikichukuliwa na Liam Lawson Oliver Bearman na Nico
Hulkenberg.

Post a Comment