DC Mpogolo Ataka Ushirikiano Kutunza Usafi Dar es Salaam
Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Mheshimiwa Edward Mpogolo, ametoa wito mzito kwa taasisi mbalimbali, viongozi wa jamii, na wafanyabiashara kuungana kwa pamoja na Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam ili kuhakikisha mji huo unabaki kuwa safi, salama, na wenye kuvutia muda wote.
Akizungumza na wadau wa usafi na mazingira leo Oktoba 10, 2026, amesisitiza kuwa dhamira ya dhati ya wakazi wa jiji hilo ni kuona usafi unafanyika kwa vitendo vya kila siku, huku kila mwananchi akitakiwa kutambua wajibu wake wa msingi wa kutunza na kupendezesha mazingira yanayomzunguka.
Katika kutilia mkazo uboreshaji huo, DC Mpogolo amewataka wadau wote kuunga mkono kwa dhati juhudi kubwa zinazofanywa na Serikali ya Awamu ya Sasa inayoongozwa na Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kuimarisha hifadhi ya mazingira.
Aiha DC huyo ametoa onyo kwa mtu au taasisi yoyote itakayokiuka taratibu zilizowekwa kwa kutupa taka ovyo au kuchafua mazingira ya jiji.
Ili kuhakikisha miundombinu inafanya kazi ipasavyo, Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam inaendelea kusimamia zoezi la usafi usiku na mchana, ikishirikiana kwa karibu na Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) katika kuzibua mitaro kwenye chemba 19 za eneo la Kariakoo ili kuondoa kero ya mfumo wa majitaka.
Pamoja na hayo, DC Mpogolo amewatahadharisha mapema wananchi wote wanaoishi katika maeneo hatarishi pembezoni mwa Mto Msimbazi kuhama mara moja ili kujiepusha na majanga ya mafuriko yanayoweza kutokea kufuatia mvua kubwa zinazotarajiwa.
Katika kuweka maneno kwenye vitendo, Wilaya ya Ilala imeanzisha zoezi kabambe la usafi wa pamoja linaloongozwa na Mheshimiwa Edward Mpogolo kuanzia mapema alfajiri ya leo.
Shughuli hiyo ya usafi imefanyika katika njia kuu nne zinazoelekea kwenye Bustani ya Benki ya NBC Makao Makuu, zikiwemo njia ya kuanzia Makutano ya Barabara ya Nkrumah na Bibi Titi kuelekea Mnara wa Askari Posta, kuanzia Makutano ya Sokoine Drive na Kilwa Road, kuanzia Eneo la Utumishi kupitia Kivukoni Front na Sokoine Drive, pamoja na kuanzia Makutano ya Bibi Titi na Maktaba. K

Post a Comment