WAGOMBEA sita wamepitishwa kugombea urais wa
Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika
Agosti 12, mwaka huu katika hatua za awali.
Akizungumza na gazeti hili Mwenyekiti wa
Kamati ya Uchaguzi, msomi
Wakili Revocatus Kuuli alitaja wagombea hao kuwa ni Shija Richard, Imani Madega, Wallace Karia, Fredrick
Mwakalebela, Ally Mayay na Emmanuel Kimbe.
“Kikao kimekaa leo na kimepitisha
majina ya wagombea kwa hatua ya awali na majina yote yatabandikwa kwenye mbao
za matangazo kuanzia kesho ,” alisema Wakili Kuuli.
Awali wagombea kumi walichukua fomu kuwania
nafasi ya urais lakini mapema Athuman Nyamlani alijitoa hivyo majina ambayo
hayakupitishwa ni Fredrick Masolwa, Jamal Malinzi na John Kijumbe kwa sababu
mbalimbali.
Katika nafasi ya Makamu wa rais waliopitishwa
ni Mulamu Ng’hambi, Michael Wambura, Mtemi Ramadhani, Stephen Mwakibolwa na Robert
Selasela huku Geofrey Nyange akielezwa kujitoa.
Katika nafasi ya wagombea wa nafasi ya kamati
ya Utendaji Kocha mwenye maneno mengi Jamhuri Kihwelo, Bakari Malima, Abdallah
Mussa, kwa kushindwa kuwasilisha cheti cha kuthibitisha elimu ya sekondari kwa
mujibu wa kanuni ya 9(2) za uchaguzi.
Wagombea ambao hawakupitishwa kwa kukosa
uzoefu kwa mujibu wa kanuni ya 9(3) ni Musa Sima, Salehe Alawi, Thabith Kandoro
na Hassan Othuman hajapitishwa kwa kukosa uadilifu kwa mujibu wa kanuni ya 9(7)
za uchaguzi wa TFF.
Zoezi la kuchukua fomu lilianza Juni 16, 2017
hadi Juni 20, mwaka huu na jumla ya
wagombea 74 walichukua na kurudisha fomu kuomba kugombea nafasi mbalimbali
katika uchaguzi huo.
Awali mchujo ulianza Juni 23, kwa mujibu wa
kanuni ya 11.1 ya Uchaguzi wa TFF lakini kulitokea kutokuelewana kati ya
mwenyekiti wa kamati hiyo Wakili Kuuli na wajumbe wa kamati hiyo hali
iliyofanya Kuuli kujiuzulu kabla ya Kamati ya Utendaji ya TFF kukaa na kuivunja
kamati hiyo na yeye kurejeshwa tena peke yake.
No comments:
Post a Comment