MHARIRI
Msaidizi wa habari za michezo wa gazeti hili, Zena Chande amechaguliwa kuwa
mjumbe wa Mkutano Mkuu wa Shirikisho la Shirikisho la Soka (TFF) katika
uchaguzi wa Chama cha Soka la Wanawake Tanzania (TWFA), ulifanyika leo Dar es
Salaam.
Zena ambae
alikuwa anatetea nafasi hiyo alipata kura 44 kati ya kura 52 zilizopigwa huku
mpinzani wake Salma Wajeso akiambulia kura nane.
Katika
nafasi ya Mwenyekiti, Amina Karuma alifanikiwa kutetea kiti chake kwa kura 47
huku kura tano zilimkataa kwani alikuwa mgombea pekee na Rose Kisiwa alitetea
nafasi yake ya Makamu Mwenyekiti kwa kura 46 na kura sita zikimkataa
Naye
mwandishi mwandamizi wa Nipashe, Somoe Ng’itu alichaguliwa kuwa Katibu Mkuu kwa
kura 49 huku kura mbili zikimkataa na katibu msaidizi alichaguliwa Theresia Mung’ong’o
kwa kura 44 na kura nane zikamkataa.
Nafasi ya
mhazini alichaguliwa Hilda Masanche kwa kupata kura 25 huku kura 24 zikimkataa
na kura tatu zikaharika na nafasi ya wajumbe wa kamati ya utendaji ilikosa watu
baada ya wagombea kushindwa kufikia nusu ya kura za wajumbe.
Wajumbe wa
kamati ya utendaji ilihitaji watu wanne na wagombea walikuwa wanne ambao ni
Triphonia Temba kura 15, Chichi Mwidege kura 12, Mwamvita
Kiyogoma kura 9 na Jasmine Soudy kura
saba.
Akizungumza wakati wa kutangaza matokeo hayo Mwenyekiti Kamati ya Uchaguzi ya
TWFA, Msomi Wakili George Mushumba, alisema wagombea hao walihitaji kupata kura
zaidi ya nusu ya wapiga kura ambao ilikuwa ni 52 ili wawe wajumbe.
“Najua
katiba inaruhusu kuteua wajumbe wawili lakini hao waliogombea wameshindwa hivyo
uongozi uliochaguliwa utaona namna inayofaa ili waweze kuendelea na kazi zao za
kuendeleza soka la wanawake,” alisema Mushumba.
Pia Mushumba
aliwashukuru wagombea na wajumbe wa mkutano huo kwa ushirikiano walioonesha kwa
kamati kipindi chote kuanza kwa mchakato wa uchaguzi na kuwataka kufanya kazi
kwa kushirikiana ili kuleta maendeleo.
Naye
Mwenyekiti wa TWFA, Amina Karuma aliwashukuru wajumbe kwa kuwarudisha
madarakani kwa kishindo na kuishukuru kamati ya uchaaguzi kwa kazi nzuri
waliyofanya kwa kusimamia uchaguzi.
“Bila
ushirikiano na ninyi sisi hatuwezi kufanya chochote hivyo naomba tuendelee
kushirikiana ili tuzidi kufanya mazuri zaidi ya hayo tuliyokwisha kufanya,”
alisema Karuma.
Uchaguzi huo
ulifanyika kwa amani na wajumbe walipiga kura mmoja mmoja kwenye chumba maalumu
baada ya kila nafasi wagombea wake kujieleza.
No comments:
Post a Comment