Viongozi hao
wamefanya hivyo kwa dhana kuu ya Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu
(FIFA) inayosisitiza uungwana katika soka ikisema: “My Game is Fair Play”. Kwa upande
wa Young Africans, uliwakilishwa na Kaimu Katibu Mkuu, Baraka Deusdedit wakati
upande wa Simba alikuwa, Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili, Zacharia Hans Poppe.
Katika kikao
hicho ambacho Msuluhishi wake, Wakili na Mwenyekiti wa zamani wa TFF wakati huo
Chama cha Mpira wa Miguu Tanzania (FAT), Said El – Maamry hakuhudhuria kwa
sababu za udhuru, Baraka wa Young Africans aliongozana na Mjumbe wa Kamati ya
Utendaji wa Young Africans, Omar Said pamoja na Mawakili Oscar Magolosa na Alx
Mushumbusi.
Kwa hali
halisi ya uchumi kwa sasa, timu hizo zimezungumza hadi kufikia mwafaka wa
kiwango kisichozidi Sh milioni 200 kutoka dola dola 600,000 (zaidi ya Sh
milioni 1,200 au Bilioni 1.2). Mazungumzo ya wikiendi hii yanakwenda
kukamilisha mvutano wao, kama ambavyo walikubaliana kwenye kikao kilichoketi
jana Novemba 03, 2016.
Madai makuu ya
Simba ni dhidi ya mchezaji Hassan Hamis Ramadhani maarufu kwa jina la Hassan
Kessy na dhidi ya Young kudaiwa kuvunja mkataba na kuingilia makubaliano mapya
wakati tayari mchezaji alikuwa na mkataba na klabu hiyo yenye maskani yake Mtaa
wa Msimbazi, Kariakoo jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment