Waandaaji wa
fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa wanawake 2016, wameipa heshima
Tanzania na kuona kuwa Twiga Stars – Timu ya Taifa ya Wanawake inafaa kuipima
ubavu kabla ya kuanza kwa fainali hizo Novemba 19, mwaka huu.
Twiga Stars
ambayo sehemu kubwa ya kikosi hicho kinaundwa na wachezaji wa timu ya taifa ya
Wanawake ya Tanzania Bara yaani Kilimanjaro Queens ina rekodi nzuri ya kuwa
kinara wa viwango vya ubora kwa nchi za Afrika Mashariki na kati lakini zaidi ni
mabinga wapya wa ukanda huo – ubingwa uliopatikana Septemba, mwaka huu huko
Uganda.
Rekodi hizo
zimesukuma Shirikisho la Mpira wa Miguu la Cameroon (FECAFOOT)
– nyumbani kwa Rais wa CAF, Issa Hayatou kuikubali Twiga Stars na hivyo kuomba
kucheza nayo mwishoni mwa wiki ijayo. Tayari Twiga Stars imeanza maandalizi ya
kutosha chini ya Makocha Sebastian Nkoma na Wasaidizi wake Edna Lema na El Uterry
Mollel.
Kutokana na
kuitikia wito huo kutakuwa na mabadiliko kidogo ya ratiba kwa Ligi Kuu ya
Waanawake. Ligi hii itaendelea kama ilivyo kwenye ratiba kwa makundi yote
mawili ya A na B, isipokuwa kwa michezo miwili tu ambayo yote ni ya Kundi A.
Mchezo kati ya
JKT Queens na Viva FC kadhalika Evergreen Queens na Mlanduzi Queens, ambayo
itapangiwa tarehe nyingine. Michezo yote hii ilikuwa ichezwe tarehe 09.11.2016
kwenye viwanja vya Karume na Uhuru, Dar es Salaam.
Timu za JKT
Queens na Mlandizi Queens zina wachezaji zaidi ya wawili kwenye Twiga Stars
ambako JKT Queens wana wachezaji 11 na Mlandizi Queens ina wachezaji watatu
No comments:
Post a Comment