SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), linatarajia
kutoa madawati 200 ikiwa ni sehemu ya mapato ya Ngao ya Hisani utakaochezwa
Agosti 17, 2016.
Akizungumza na wandishi wa habari, Afisa habari wa
TFF, Alferd Lucas, alisemna TFF inaunga mkono juhudi za Bunge la Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania na juhudi za Serikali kwa katika kuhakikisha vijana wa
Kitanzania wanakuwa na mazingira bora ya kupata elimu.
“TFF imeona umuhimu wa kusaidia elimu ya Tanzania ndio
maana imeamua
kutoa sehemu ya mapato yake kama mchango wa kusaidia
madawati kupitia mchezo wa ngao ya jamii utakaochezwa Agosti 17 kuashiria msimu
mpya wa Ligi Kuu”, alisema Lucas.
Pia Lucas alisema TFF inamshukuru Katibu Mkuu wa Bunge, Dkt.
Thomas Kashililah kwa juhudi za kuendelezaa mpira wa miguu na kuutumia katika
kuliletea Taifa maendeleo.
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania litaendelea
kushirikiana na Ofisi ya Bunge Sports Club katika kufanikisha mashindano
mbalimbali hasa mchezo wa Hisani kati ya Simba Sports Club na Young African
(Wabunge) utakaofanyika hapo baadaye kwa mujibu wa ratiba na uratibu wa Bunge.
Mchezo wa Ngao ya Jamii utazikutanisha Yanga na Azam
FC na utachezwa Agosti 17 kwenye Uwanja wa Taifa kuashiria msimu mpya wa Ligi
Kuu Tanzania Bara.
No comments:
Post a Comment