RAIS wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF),
Jamal Malinzi, amewataka makocha wanaoshiriki kozi ya ukocha wa leseni A,
kwenda kutumia elimu hiyo kusaidia na kuendeleza soka.
Malinzi aliyasema hayo jana wakati akifungua kozi hiyo
ambayo inashirikisha makocha 20 na kufanyika kwenye Uwanja wa Karume, Dar es
Salaam.
“Ndugu zangu makocha nawasihi mnapohitimu kozi hii
msiende kuweka vyeti vyenu ndani bali mkawe chachu ya mafanikio ya soka kwani
kwa idadi ya makocha 23 ambao wana leseni A ni makocha saba tu ambao
wanafundisha”, alisema Malinzi.
Pia Malinzi alisema ikimaliza kozi hii Tanzania
itakuwa na makocha 43 wenye leseni A jambo ambalo ni idadi ndogo ikilinganishwa
na Tanzania ambayo ina watanzania milioni 50.
Pia Malinzi alisema kuanzia msimu huu mpya wa ligi
makocha watakaoruhusiwa kuwa na timu za ligi kuu ni wale wenye leseni A na kwa
daraja la kwanza ni wenye leseni B huku akisema wasaidizi watatakiwa kuwa na
leseni C.
Kozi hii itakuwa inafendeshwa na mkufunzi Sunday
Kayuni akisaidia na Salum Madadi na itakuwa ya mwezi mmoja lakini ikimalizika
wiki mbili itasimama na kuja kumalizika Novemba, 2016.
No comments:
Post a Comment