Aina 13 za tuzo ya Ligi hiyo inayodhaminiwa na kampuni ya mawasiliano ya Vodacom Tanzania zilitolewa kwa washindi chini ya uratibu wa Kamati ya Tuzo ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) inayoundwa na waandishi wa habari za michezo, makocha, viongozi (administrators) na wawakilishi kutoka kwa wadhamini (Vodacom na Azam Tv).
Tuzo hizo na zawadi yake ya fedha kwenye mabano zilikwenda kwa Young Africans SC walioibuka mabingwa wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara msimu wa 2015/2016 hivyo kuvuna Sh. 81,345,723 wakati Mshindi wa pili ni Azam aliye Sh. 40,672,861 wakati mshindi wa tatu alikuwa ni Sh. 29,052,044 huku Tanzania Prisons ilivuna Sh. 23,241,635 kwa kushika nafasi ya nne.
Mtibwa Sugar iliibuka timu yenye Nidhamu Bora na kupata Sh. 17,228,820. Mtibwa ilizishinda timu za JKT Ruvu na Mgambo Shooting na wakati mfungaji bora alikuwa Amisi Tambwe wa Young Africans aliyevuna Sh. 5,742,940 kiasi ambacho kinafafa na alichozawadiwa Aishi Manula wa Azam. Manula aliwashinda Beno Kakolanya wa Tanzania Prisons na Deogratius Munishi wa Young Africans.
Pia kiasi kama hicho cha Sh. 5,742,940 hicho kilikwenda kwa Thabani Kamusoko wa Young Africans aliyeibuka Mchezaji Bora wa Kigeni baada ya kuwashinda Donald Ngoma wa Young Africans na Vincent Agban wa Simba. Pia Mwamuzi Bora, Ngole Mwangole alipata Sh. 5,742,940. Mwangole aliwawashinda Anthony Kayombo na Rajab Mrope.
Hans Van Pluijm wa Young Africans alishinda tuzo ya Kocha Bora na kuvuna Sh 8,000,000 baada ya kuwazidi kura Mecky Maxime wa Mtibwa Sugar na Salum Mayanga wa Tanzania Prisons wakati Mchezaji Bora Chipukizi aliteuliwa ni Mohamed Hussein wa Simba na kujivunia Sh. 4,000,000. Hussein aliwashinda Farid Mussa (Azam), Mzamiru Yasin (Mtibwa Sugar) na Shiza Kichuya (Mtibwa Sugar).
Wakati Ibrahim Ajib akishinda tuzo na Sh 3,000,000 kama mfungaji Goli bora la msimu kwa kumshinda Amisi Tambwe wa Young Africans, Juma Abdul aliwashinda Shiza Kichuya (Mtibwa Sugar) na Mohamed Hussein (Simba). Abdul alipewa tuzo na zawadi ya Sh. 9,228,820.
KAULI YA MALINZI
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi alianza kutoa historia ndefu ya soka la Tanzania kwamba limetoka mbali KWA viongozi waliopita kufanya kazi katika mazingira magumu na kufanikiwa, maendeleo ambayo imekuwa chachu ya uongozi wa sasa.
Rais Malinzi alichukua nafasi hiyo kuomba radhi wadau wa soka kwamba pangapangua ya ratiba haitakuwa kwa kiasi kikubwa msimu wa 2016/2017 ingawa kwa msimu uliopita haikufanyika kwa makusudi. “Tutajitahidi kutopangua ratiba.”
Rais Malinzi aliyetumia muda mwingi kuishukuru Vodacom kwa hatua wanayopiga kusogeza mbele soka la Tanzania, alielekeza kwamba si vema kufananisha Ulaya na Afrika hususani Tanzania ambako miundombinu inachangamoto kubwa hivyo kuwataka kuchambua ukweli huo badala ya umma kupotoshwa.
Alifafanua ya uwepo wa kanuni mpya wa Ligi Daraja la Kwanza kwamba itaendesha soka ka uweledi zaidi hivyo kukwepa upangaji wa matokeo. “Tusiingie kwenye dhambi ya rushwa na upangaji wa matokeo kwenye ligi na club licensing itatusaidia. Lakini klabu itakayokuwa na tatizo, hakutakuwa na msamaha.”
MWIGULU NCHEMBA
Naye Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Lameck Nchemba, aliipongeza TFF kwa mafanikio na ubunifu na usimamizi wa soka la Tanzania. Alitaka wadau kuwa na imani na TFF ambayo inapambana na rushwa katika soka kwa ligi mbalimbali inazozisimamia ili kujenga timu bora ya taifa –Taifa Stars.
No comments:
Post a Comment