FC PORTO 4 vs 0 FC BASEL (Agg 5-1)
FC Porto wameitandika FC Basel Bao 4-0 katika Mechi ya Marudiano ya Raundi ya Mtoano ya Timu 16 ya UEFA CHAMPIONS LIGI iliyochezwa huko Ureno.
Katika Mechi ya kwanza huko Uswisi, Timu hizi zilitoka Sare ya 1-1.
Mchezaji wa Kimataifa wa Algeria Yacine Brahimi alifunga Bao kwa Frikiki safi ya Dakika ya 14 na kuwafungulia milango FC Porto ambao Kipindi cha Pili, FC Porto walipiga Bao 3 nyingine kupitia Hector Herrera, Frikiki safi ya Carlos Casemiro na Goli la Ruben Neves.
Bao...!
FC Porto imetinga Robo Fainali kwa Jumla ya Mabao 5-1 na itajua mpinzani wake hapo Machi 20 Droo itakapofanyika.
No comments:
Post a Comment