GOLIKIPA wa
Yanga Juma Kaseja na waajiri wake Yanga limechukua sura mpya baada ya kutakiwa
kumalizana nje ya mahakama.
Kesi hiyo ambayo iliendelea leo katika Mahakama ya Kazi baada ya Februari 12 kuahirishwa kutokana na wakili anayemsimia mlinda mlango huyo Samson Mbamba kuunguliwa ofisi yake ambapo nyaraka mbali mbali zikiwemo za Kaseja kuungua na kuomba kupewa upya nyaraka nyingine na kesi hiyo kuendelea leo.
Kesi hiyo ambayo inasuluhishwa na Muheshimiwa Alfred Massey, aliwataka Yanga kumalizana na Kaseja nje ya mahakama na kesi hiyo itaendelea tena Machi 16 saa sita mchana kuangalia iwapo pande zote mbili zimeridhia na kutekeleza masharti waliyopewa.
Katika masharti hayo Kaseja anatakiwa kutaja kiasi gani cha fedha ambacho anaweza kuilipa Yanga huku klabu hiyo nayo ikitakiwa kuangalia kama itaweza kumrudisha kundini Kaseja.
Wakili wa Yanga Frank Chacha, akizungumzia suala hilo alisema "Kuna masharti tumepewa pande zote mbili, masharti ambayo ni siri hatutakiwi kusema kwa vile ni usuluhishi ndio maana hata nyinyi mmezuiwa kuingia kusikiliza, ninachoweza kusema tumeridhia kwa pamoja pande zote kukaa na kumaliza hili suala nje ya mahakama, na hiyo Machi 16 tutarudi kwa ajili ya kueleza muafaka tuliofikia."alisema Chacha.
Kaseja alipanda kizimbani kwa mara ya kwanza Februari 12 kwenye Tume ya Usuluhishi na Uamuzi iliyo chini ya Mahakama ya Kazi kwa lengo la kujibu shtaka la kuvunja mkataba ikiwa ni pamoja na kuilipa Yanga kiasi cha Sh 340 milioni. Hata hivyo, Kaseja alipelekwa katika hatua ya usuluhihi ili kujibu kama yuko tayari kulipa fidia au vipi na kama hakutakuwa na muafaka kesi hiyo itapelekwa kwenye hatua ya uamuzi ambayo ni sawa na kesi nyingine.
Uongozi wa Yanga uliingia kwenye uhasama na kipa, Juma Kaseja ‘Tanzania One’ baada ya kumtaka kipa huyo kuwalipa fidia ya Sh340 milioni, baada ya mlinda mlango huyo kuandika barua Novemba 11 ya kuvunja mkataba na wanajangwani hao, hata hivyo uongozi huo chini ya Yusuf Manji ulipitia barua hiyo ya Kaseja na kumjibu Desemba 15 ikiwa ni mwisho wa dirisha dogo la usajili ikitaka kiasi hicho cha fedha.

No comments:
Post a Comment