Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Friday, July 11, 2014

WACHEZAJI WALIKATAA KUPIGA PENATI YA MWANZO - VAN GAAL.


KOCHA wa timu ya taifa ya Uholanzi, Louis van Gaal amedai kuwa wachezaji wake wawili katika kikosi chake walikataa kuchukua jukumu la kupiga penati ya kwanza katika mchezo wa nusu fainali ya Kombe la Dunia dhidi ya Argentina ambao uliamuliwa kwa changamoto hiyo. 
Beki Ron Vlaar alijitokeza kupiga penati hiyo lakini kipa wa Argentina Sergio Romero aliokoa penati hiyo na kupelekea Argentina kushinda kwa penati 4-2 katika mchezo huo na kutinga fainali ya michuano hiyo ambapo sasa watakwaana na Ujerumani Jumapili. 
Akihojiwa mara baada ya mchezo huo, Van Gaal amesema aliwataka wachezaji wawili kupiga penati kabla ya kumchagua Vlaar kwaababu alidhani alikuwa mchezaji mzuri ndani ya uwanjani hivyo anaweza kuwa anajiamini. Lakini mambo yalikuwa tofauti na hiyo inaonyesha jinsi gani changamoto ya mikwaju ya penati ilivyokuwa sio kitu rahisi.

No comments:

Post a Comment