Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Wednesday, July 9, 2014

Samuel Eto’o kurejea tena nchini Italia mara hii ni AS Roma endapo mambo yatakwenda poa


Samuel Eto’o kuelekea Italia
KLABU ya AS Roma ya Italia imeanza mazungumzo na wawakilishi wa Samuel Eto’o jana ikiwa ni baada ya kukamilisha usajili wa mchezaji mwenzake wa zamani wa Chelsea Ashley Cole.
 Eto’o mwenye umri wa miaka 33 ni mchezaji huru toka aondoke Stamford Bridge na tayari amepata ofa kutoka China na Uturuki lakini mwenyewe anataka kurejea nchini Italia. 
Katika mazungumzo hayo nyota huyo anatarajiwa kupunguziwa mshahara wake kwa kiasi cha paundi milioni tatu ikiwemo na posho.
 Kama akifanikiwa kutua Roma atakuwa amejiunga na mchezaji mwenzake kutoka Chelsea, Cole aliyesaini mkataba wa miaka miwili na timu hiyo huku ikiwa ni mara ya pili kwa nyota huyo kurejea nchini Italia baada ya kuitumikia Inter Milan kati mwaka 2009 na 2011.

No comments:

Post a Comment