ARSENE WENGER: KUTUA KWA ALEXIS SÁNCHEZ NI KUVUNA MAKOMBE TU
Sanchez, mwenye Miaka 25, amesaini Mkataba wa muda mrefu unaosadikiwa kuwa wa Miaka Mitano baada kufuzu upimwaji Afya yake uliofanyika Leo Jijini London kwenye Kituo cha Mazoezi cha Arsenal cha Colney.
Awali iliaminika Sanchez atakwenda Liverpool kwenye Dili inayomhusisha Luis Suarez kuihama Liverpool na kwenda Barcelona lakini Mchezaji huyo aliamua angependa kujiunga na Arsenal.
Akimkaribisha huko Emirates, Meneja wa Arsenal, Arsene Wenger, amesema Mchezaji huyo ataongeza nguvu, ubunifu na ubora katika azma yao ya kutwaa Ubingwa ambao wameukosa kwa zaidi ya Miaka 10 sasa.
Arsenal wanatarajiwa pia kumnasa Beki wa France anaecheza Newcastle, Mathieu Debuchy, kwa Dau la Pauni Milioni 11 huku Wenger akiwawinda Loic Remy wa QPR na Kiungo wa Germany Lars Bender.
Post a Comment