SUNDERLAND YAIFUNGA NEWCASTLE UNITED 3-0, WAFUNGAJI NI BORINI, ADAM JOHNSON NA JACK COLBACK
Sunderland waichapa tena Newcastle leo
kwenye ligi kuu England EPL. Msimu huu wa 203/14 , katika Mechi ya
kwanza chini ya Gus Poyet waliichapa Newcastle Bao 2-1.
Newcastle wakiwa kwao kwenye uwanja wa St. James' Park wakicheza bila Kiungo Yohan Cabaye amabaye amehamia Paris Saint-Germain na pia Straika Loic Remy ambae yupo Kifungoni baada Kadi Nyekundu kwenye Mechi ya Jumanne iliyopita na Norwich.
Bao za Sunderland leo zimefungwa na Fabio Borini likiwa ni bao la mkwaju wa penati katika dakika ya 19 na bao la pili likifungwa na Adam Johnson katika dakika ya 23 kipindi hicho hicho cha kwanza. Newcastle walionekana kutokuwa makini kwenye mtanange huu ambapo pia wamekosa nafasi za wazi nyingi. Dakika ya 80 kipindi cha pili Jack Colback ameiongezea bao Sunderland na kufikisha bao 3-0 dhidi ya wenyeji Newcastle United waliokuwa kwao kwenye uwanja wa St. James' Park. Ushindi huu umewapandisha sana Sunderland kwenye msimamo huo wa ligi wakiwa na pointi 24 na kupanda hadi nafasi ya 12 kutoka katika nafasi ya 17. Wakati wao Newcastle United wamebakia hapo hapo katika nafasi ya 8 wakiwa na pointi zao 37.
Nyomi kuelekea kwenye uwanja wa St. James Park
Makocha wote wawili wakisalimiana kabla ya mtanange
Borini akichonga mkwaju wa penati.
Kipa wa Newcastle hakuona ndani kwa mkwaju huo wa Borini. Sunderland walianzia hapa kupata bao na kufanya 1-0.
Shangilia ya Borini Noma leo hii...
Adam Johnson akifunga la pili
Tulieni.....2-0
Majanga!!!
Sundeland
wakiongoza mashambulizi..na kufanikiwa kupata bao la tatu na mpira
kumalizika kwa 3-0 kwenye uwanja St. James Park leo.
RATIBA/MATOKEO
Jumamosi Februari 1
Newcastle 0 vs Sunderland 3
West Ham 2 vs Swansea 0
18:00 Cardiff vs Norwich
18:00 Everton vs Aston Villa
18:00 Fulham vs Southampton
18:00 Stoke vs Man Utd
18:00 Hull vs Tottenham

Post a Comment