Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Saturday, February 15, 2014

JOSE MOURINHO NA ARSENE WENGER WAPONDANA KWA KUJIBISHANA

Huko England leo zimepambwa na Mipasho kati ya Mameneja wa Chelsea na Arsenal, Jose Mourinho na Arsene Wenger, ambao walikuwa wakijibizana maneno ikiwa sasa ni dhahiri lile joto la mbio za Ubingwa limezidi kupamba moto.
Kwenye Ligi Kuu England, Chelsea ndio wanaongoza wakiwa Pointi 1 mbele ya Arsenal ambao wako Pointi 2 mbele ya Man City waliocheza Mechi moja pungufu huku Liverpool wakiwa Nafasi ya 4 Pointi 1 nyuma ya City.

Akijibu kauli ya Arsene Wenger kwamba Msimu huu Ubingwa ni wa Chelsea labda waupoteze, Jose Mourinho, Meneja wa Chelsea, alitoa kauli kali mno aliposema: “Wenger ni Bingwa wa Kufeli. Mimi sio. Kama yupo sawa kwamba mimi naogopa kushindwa ni kwa sababu mie sishindwi mara nyingi!”

Chini ya Wenger, Arsenal haijatwaa Kombe tangu 2005 walipotwaa FA CUP na Mourinho aligusia hilo: “Miaka 8 bila Kombe, huko ni kufeli!”

Akiwa na Chelsea kati ya Miaka ya 2004 na 2007, Mourinho alitwaa Ubingwa wa Ligi Kuu mara 2, na pia kutwaa Mataji ya Ubingwa katika Nchi 4 tofauti pamoja na UEFA CHAMPIONZ LIGI akiwa na FC Porto na Inter Milan.

Mourinho aliongeza: “Ukweli ni kuwa yeye ni Bingwa wa Kufeli kwa sababu Miaka 8 bila Kombe huko ni kufeli. Nikifanya hivyo nikiwa na Chelsea, Miaka 8, nitaondoka na sirudi tena!”

Chelsea na Arsenal zitakutana kwenye Ligi hapo Machi 22 Uwanjani Stamford Bridge kwenye Mechi ambayo, bila shaka, itakuwa muhimu mno kwenye mbio za Ubingwa.


Mara ya kwanza kukutana huko Emirates kwenye Ligi Msimu huu hapo Desemba 23, Arsenal na Chelsea zilitoka 0-0.

No comments:

Post a Comment