Tafca yasubiri uchaguzi kusonga mbele
KATIBU wa Shirikisho la sanaa na Ufundi Tanzania (TAFCA), Marco Tibasima amesema shirikisho hilo linasubiri kukamilika kwa mchakato wa uchaguzi ili kuweza kuanzisha rasmi programu na shughuli zingine za maonesho.
Akizungumzia mchakato huo, Tibasima amesema uchaguzi huo unatarajiwa kufanyika mwezi ujao, huku wanachama wakiwa katika maandalizi ya kusubiri bodi itamke tarehe rasmi ya uchaguzi ili kupata uongozi mpya utakaosimamia maslahi ya shirikisho hilo.
ma amesema uchaguzi huo unatarajiwa kufanyika mwezi ujao, huku wanachama wakiwa katika maandalizi ya kusubiri bodi itamke tarehe rasmi ya uchaguzi ili kupata uongozi mpya utakaosimamia maslahi ya shirikisho hilo.
Ameongeza kuwa shirikisho lina mambo mengi ya kimkakati ya kufanya kwa ajili ya ustawi wa wanachama wake, na kwamba baada ya uchaguzi kukamilika, masuala ya mafunzo na maonesho yatashika kasi kubwa ili kuwakwamua wasanii kiuchumi.
Sambamba na mipango hiyo ya baada ya uchaguzi, TAFCA inatarajia kushirikiana na Tanzania International Tourism Festival (TITF) kuandaa tamasha kubwa la kitaifa Oktoba mwaka huu, litakalowakutanisha wachongaji, wachoraji, wabunifu wa mavazi, watengenezaji wa vito, wafinyanzi na wasanii wengine wa kazi za mikono kutoka maeneo mbalimbali nchini.
Tamasha hilo la sanaa na kazi za ufundi linalenga kuipa sekta ya utalii na sanaa nchini msukumo mpya, likiwa na dhamira ya kuhamasisha uchumi wa ubunifu, kutangaza utamaduni wa Tanzania na kuwafungulia wasanii masoko ya ndani na kimataifa.
Akizungumzia maandalizi hayo Mkurugenzi wa TITF, Ibrahim Jamal alieleza kuwa tamasha hilo limebeba maono ya kuunganisha sekta ya sanaa na utalii ili kuongeza thamani ya kazi za ubunifu na kuwapatia wasanii fursa za kibiashara, zikiwemo mafunzo ya uongezaji thamani wa bidhaa, ulinzi wa haki za kazi za ubunifu, na mbinu za kufikia masoko ya nje.

Post a Comment