WAKATOLIKI WASEMA WALICHOZUNGUMZA NA SAMIA
Baraza la
Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) limesema mkutano waowa hivi karibuni na Rais Samia Suluhu Hassan uliombwa nao kwa lengo kuu la kumkabidhi
andiko maalum linaloeleza mtazamo wao kuhusu hali ya kisiasa nchini .
Pia wanasema
waraka waliokabidhi umelenga pia kuzungumzia uimarishaji wa mazungumzo ya
kitaifa yanayolenga kujenga amani, ukweli, msamaha na uponyaji wa taifa.
Katibu Mkuu wa
TEC, Padri Dk Charles Kitima, alisema hayo kupitia picha jongefu iliyosambazwa
kwa umma kuhusu mazungumzo yaliyofanyika kati ya maaskofu na Rais Samia jijini
Dodoma, Agosti 10, 2026.
Alieleza kuwa
hatua hiyo ya kutaka kumuona Rais Samia ilitokana na azimio la kikao cha mwaka
cha maaskofu kilichofanyika mwezi Juni, ambapo viongozi hao waliona umuhimu wa
kuendelea na mazungumzo yaliyoanza mwaka uliopita ili kutimiza wajibu wao wa
kimaadili wa kuelimisha jamii kuhusu utu, upendo, na kuishi kindugu.
Kupitia
mazungumzo hayo, maaskofu walisisitiza kuwa mazungumzo na kukiri ukweli ni njia
muhimu ya kuvuka migogoro kama inavyoshuhudiwa katika nchi nyingine duniani,
huku wakikumbusha wajibu wa viongozi wa dini katika kuhamasisha amani na
kuheshimu utu wa binadamu chini ya mamlaka ya maamuzi na utekelezaji iliyo
mikononi mwa serikali.
Aidha, TEC
imeahidi kuendelea kushirikiana na serikali na wadau mbalimbali ili kuhakikisha
utulivu na mshikamano wa Watanzania unadumishwa.

Post a Comment