VYOMBO VYA HABARI VYA ULAYA VYASIFU TUME YA UCHUNGUZI YA TANZANIA

 


Baadhi ya vyombo vya habari vya kimataifa barani Ulaya vimeeleza kuridhishwa na hatua ya serikali ya Tanzania ya kuunda tume huru inayoongozwa na Jaji Shabani Ally Lila kuchunguza kwa kina matukio ya vurugu yaliyotokea wakati na baada ya uchaguzi mkuu.

Vyombo hivyo vimeeleza kuwa kuundwa kwa Tume hiyo ni hatua inayolenga kuondoa mijadala ya kisiasa na kurejesha uchunguzi katika ushahidi, sheria na uwajibikaji.

Miongoni mwa vyombo hivyo ni gazeti la Indegazette la Ubelgiji na shirika la habari la The News Agency lenye makao yake Brussels, ambavyo vimeangazia muundo wa Tume hiyo yenye majaji kutoka Tanzania, Namibia na Uganda.

Vyombo hivyo vimeeleza kuwa uzoefu mpana wa majaji hao unaweza kusaidia kujenga uaminifu katika mchakato wa uchunguzi.

Hatua ya Rais Samia Suluhu Hassan kuunda Tume hiyo imeelezwa kuwa inaonyesha Tanzania iko tayari kuchunguza yaliyotokea kwa kutumia taasisi, sheria na ushahidi ili kupata majibu.

No comments