Arsenal wako Nafasi ya Pili kwenye Msimamo wa Ligi Kuu England wakiwa Pointi 1 nyuma ya Vinara Chelsea lakini katika Mechi zao mbili zilizopitwa walibondwa Bao 5-1 na Liverpool huko Anfield na kutoka Sare 0-0 na Manchester United Uwanjani Emirates.
Wenger amesema Wachezaji wake wako makini na wanatilia mkazo mbio za Ubingwa huku Mechi zikiwa zimebaki 12.
Wenger ametamka: “Ukitamka haumo kwenye mbio za Ubingwa, basi huwezi kupoteza Ubingwa. Ni jambo rahisi tu. Kazi yetu ni kuwa na matarajio makubwa na kujaribu kutwaa Ubingwa. Kama hatushindi, basi unawajibika kwa kuchukua lawama zote.”
Aliongeza: “Tupo kwenye kinyang’anyiro cha Ubingwa. Tutajaribu na kutoa nguvu zetu zote. Kama hatuwi Bingwa, nitawajibika!”
Mechi inayofuata kwa Timu ya Arsenal kwenye Ligi kuu ni Jumamosi February 22 na Sunderland na kwenye FA Cup kesho kutwa anakutana na Liverpool tena.
LIGI KUU ENGLAND
RATIBA MECHI ZIJAZO:
Jumamosi Februari 22
15:45 Chelsea v Everton
18:00 Arsenal v Sunderland
18:00 Cardiff v Hull
18:00 Man City v Stoke
18:00 West Brom v Fulham
18:00 West Ham v Southampton
20:30 Crystal Palace v Man United
Jumapili Februari 23
16:30 Liverpool v Swansea
16:30 Newcastle v Aston Villa
19:00 Norwich v Tottenham
No comments:
Post a Comment