Kumekucha Ligi Kuu Bara 2026/27
MSIMU mpya wa Ligi Kuu Tanzania Bara 2026/2027 unaanza rasmi leo huku mechi tatu zikitimua vumbi katika viwanja tofauti.
Ligi hiyo inaanza baada ya mechi ya ufunguzi wa msimu ya Ngao ya Jamii kuchezwa ambapo Yanga iliifunga Simba kwa bao 1-0 kwenye Uwanja wa New Amaan Complex, Unguja, Zanzibar juzi.
Katika mchezo namba moja, Pamba itafungua dimba kwa kuikaribisha Dodoma Jiji kaika Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.
Huo ni mchezo wa kipekee wa ufunguzi kwani Pamba Jiji watataka kuonesha ushindani dhidi ya Dodoma Jiji chini ya benchi lao jipya la ufundi.
Mechi hiyo inatarajiwa kuwa na ushindani mkali wa mbinu huku Pamba wakisukumwa na mashabiki wa Kanda ya Ziwa. Mbeya City watakuwa Uwanja wa Sokoine, Mbeya kuikabili Geita Gold waliopanda daraja msimu huu.
Mchezo mwingine utakuwa kati ya Singida Black Stars dhidi ya Fountain Gate, Uwanja wa Airtel.

Post a Comment