MSHAMBULIAJI wa Kimataifa wa Yanga, Hamis Kiiza ni miongoni
mwa wachezaji watatu waliongezwa kwenye kikosi cha Uganda kitakachoshiriki
mashindano ya CECAFA yanayotarajiwa kuanza Novemba 27, mwaka huu jijini
Nairobi.
Kocha wa Uganda Mulitin
‘Micho’ Sredojevic juzi aliongeza wachezaji watatu wanaocheza soka la kulipwa
nje ya Uganda ili kukipa nguvu kikosi hicho ambacho kina wachezaji 20 sasa.
Wachezaji
ambao wameongezwa ni Aucho
Khalid na Daniel Sserunkuma ambao wanacheza soka lao nchini Kenya katika timu
za Tusker FC na Gor Mahia FC pamoja na Hamis Kiiza anayechezea Yanga ya Dar es
Salaam.
Awali Micho alisema hatatumia mchezaji ambaye anacheza soka
nje ya Uganda kwa sababu anajenga timu itakayoshiriki fainali za mashindano ya
Afrika kwa wachezaji wanaocheza ndani yatakayofanyika Afrika Kusini 2014 lakini
kwa sasa ameamua kuwaweka ili wasaidie kuleta changamoto katika mashindano ya
CECAFA.
Kikosi
kamili cha Uganda ni makipa ni Ochan Benjamin, Ismail Watenga na Franco Oringa
.
Mabeki ni
Julius Ntambi, Nicholas Wadada, Isaac Muleme, Godfrey Walusimbi, Richard
Kasagga, Savio Kabugo, Ibrahim Kizza
na Martin Mpuga.
Viungo ni
Khalid Aucho, Geoffrey ' Baba ' Kizito, Said Kyeyune, Joseph Mpande, Brian
Majwega na Vincent Kayizzi
Washambuliaji
ni Hamis ' Diego ' Kiiza , Emmanuel Okwi na Dan Sserunkuma na benchi la ufundi linaundwa na Mulitin '
Micho ' Sredojevic ( Kocha Mkuu ), Kefa Kisala ( kocha msaidizi ) , Fred Kajoba
(Kocha wa makipa), Crispus Muyinda
(Meneja wa timu) na Dk Ronald Kisolo pamoja na Media afisa Kenneth Muwanga .
Uganda
Cranes ipo kundi C pamoja na Rwanda, Sudan na Eritrea na itaanza kutetea
ubingwa wake dhidi ya Rwanda Novemba 29 mwaka huu.
No comments:
Post a Comment