Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Thursday, September 12, 2013

KIBADENI AAHIDI KULIPA DENI LA MTIBWA

KATIKA hali ya kutaka kuondoa ‘uteja’ wa kufungwa na Mtibwa mara mbili kwenye msimu wa Ligi Kuu uliopita, Kocha Mkuu wa timu ya Simba, Abdallah Kibadeni, amesema lazima katika mechi ijayo ahakikishe wanalipiza kisasi.

Simba watakuwa wenyeji wa Mtibwa Sugar katika mchezo utakaofanyika katika Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam Septemba 14, mwaka huu.
Akizungumza jijini Dar es Salaam, kocha huyo alisema kuwa silaha zote wanazozitegemea Mtibwa anazifahamu na kwamba atahakikisha anatumia zilaha zake kila mbinu kuwaangamiza.

“Mtibwa Sugar si lolote kwetu, kwa sababu nafahamu mbinu  zao na pia wachezaji wao tegemeo, hivyo lazima  katika mechi ijayo  tuibuke  na ushindi mnono pamoja na kuwapa raha mashabiki," alisema Kibadeni
 Aidha kocha huyo aliwataka mashabiki na wapenzi wa Simba kuwa wavumilivu, ili kutoa nafasi kwake kuleta mabadiliko katika timu hiyo msimu huu na kurudisha hadhi yao kama ilivyokuwa zamani.

Simba inaingia uwanjani kupambana na Mtibwa Sugar, ikiwa na kumbukumbu ya kufungwa jumla ya mabao 3-0, baada ya mechi ya kwanza wakata miwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 mjini Morogoro na mchezo wa pili waliibuka na ushindi wa bao 1-0 jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment