Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Thursday, September 12, 2013

JONAS MKUDE NA JERRYSON TEGETE WAFUKUZIA KIATU CHA DHAHABU

WASHAMBULIAJI wawili, Jerryson Tegete wa Yanga na Jonas Mkude wa Simba, wameahidi ahadi zinazofanana, huku wakiwa na uwiano sawa wa mabao waliyofunga katika michuano ya Ligi Kuu Bara.

Mkude alilsema hivi karibuni kwamba kasi yake ya kupachika mabao aliyoianza katika klabu yake ya Simba ataiendeleza ili kutimiza ndoto za kuwa mfungaji bora msimu huu.

Ahadi kama hiyo ilitolewa pia na Tegete, ambaye naye alilithibitisha nia yake ya kuhakikisha anakuwa mfungaji bora ili kurudisha kasi yake ya siku za nyuma.

Hadi sasa wachezaji hao kila mmoja amepachika mabao mawili ambapo Mkude aliifungia Simba mabao yote mawili na kupata matokeo ya sare ya 2-2, wakati timu hiyo ilipocheza mchezo wa fungua dimba  dhidi ya Rhino FC ya Tabora.

Mchezo huo ulipigwa Agosti 24 katika Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi, mjini Tabora.
Tegete naye alipachika mabao mawili katika mechi yao ya ufunguzi, iliyoikutanisha Yanga na Ashanti, ambapo Yanga ilipata ushindi wa mabao 5-1.

Mpaka sasa wafungaji watatu, Tegete, Mkude na Bakari Kondo wa JKT Ruvu ndio waliokwisha pachika mabao mawili kila mmoja.
Wafungaji wengine walioambulia bao moja kila mmoja ni Haruna Niyonzima, Nizar Khalfan na Simond Msuva kutoka Yanga.

Wengine ni Juma Luizio (Mtibwa), Agrey Moris (Azam), Abdi Banda (Coastal) na Jerome Lembele (Ruvu Shooting).

Matokeo ya Ligi Kuu kwa sasa kabla haijaanza tena Septemba 14 ni Yanga 5-1 Ashanti, Rhino Rangers  2-2 Simba SC, Mbeya City     0-0 Kagera Sugar, Ruvu Shooting 3-0 Prisons FC, JKT Oljoro 0-2 Coastal Union, Mtibwa Sugar 1-1 Azam FC, Mgambo Shooting 0-2 JKT Ruvu, Yanga SC 1-1 Coastal Union, Rhino Rangers  0-2 Azam FC, JKT Oljoro 0-1 Simba SC, Mgambo Shooting  1-0 Ashanti UTD, Mtibwa Sugar 1-0 Kagera Sugar, Mbeya City 2-1 Ruvu Shooting, JKT Ruvu 3-0 Prisons FC

Timu vigogo katika Ligi hiyo, Simba na Yanga zinaingia tena viwanjani Septemba 14, ambapo Yanga itakwenda jijini Mbeya kuivaa Mbeya City, wakati Simba itavaana na Mtibwa katika mechi itakayochezwa kwenye Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment