Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Thursday, September 12, 2013

MBEYA CITY YAIPIA YANGA

TIMU ya Mbeya City iliyopanda daraja msimu huu, imedai kuwa imejipanga vizuri kuivaa Yanga. Timu hizo zitaumana Septemba 14, katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara utakaochezwa kwenye Uwanja wa Sokoine, mjini Mbeya.

Kocha Mkuu wa Mbeya City, Juma Mwambusi, ameliambia DIMBA kuwa anaijua vizuri timu ya wapinzani wao kwa vile haina mabadiliko sana na ile iliyocheza msimu uliopita, hivyo amejipanga kuhakikisha wanapata ushindi katika uwanja wao wa nyumbani.

Katika harakati hizo, Mbeya City juzi katika Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine, ilijipima nguvu kwa timu ya Kimondo ya Mbozi, inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza.
Katika mchezo huo, Mbeya City ilifanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-1, ambao Mwambusi alisema licha ya ushindi huo kutokuwa na faida kwa vile ni wa mechi ya kirafiki, lakini ameweza kubaini mapungufu na kuyafanyia kazi.

Alisema anatambua kwamba timu hiyo itahitaji ushindi ili iweze kujiweka sawa katika harakati za kutetea ubingwa wao, lakini na timu yake nayo ina kazi kubwa ya kuwahakikishia mashabiki wake kwamba hawakupanda daraja msimu huu kwa kubebwa.
"Tunatakiwa tushinde ili tulipe deni la mashabiki wetu, wametuamini na hatutowaangusha," alisema kocha huyo.

No comments:

Post a Comment